Binti aliyegoma kuolewa adaiwa kuuawa kinyama

MAUAJI

Binti Nanyoli Mohee (14) mkazi wa Kijiji cha Endepes, wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha, anadaiwa kuuwawa kwa kupigwa fimbo mbele ya baba yake mzazi, katika harakati za kumlazimisha kuolewa. Taarifa za tukio hilo zimetolewa na uongozi wa Mtandao wa Utetezi wa Haki za watoto, wanawake na wasichana (TAPO) ukisema kuwa limetokea mwanzoni mwa wiki hii katika kijiji cha Endepes.

Mmoja wa viongozi wa TAPO, Neema Laizer akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha amesema mwanaume aliyetambulika kwa jina la Amyor Matayo alimshambulia binti huyo kwa kumpiga na fimbo mbele ya baba yake mzazi akimlazimisha kumpeleka nyumbani kwake kama mke kwa kuwa alishamlipia mahari alipokuwa mdogo.

“Binti aligoma kuondoka kwenda kuolewa ndipo baba yake alimtaka mumewe amchape kwa fimbo,”anasema Laizer na kuongeza kuwa awali binti huyo alichukuliwa na mwanaume huyo kwa ajili ya maisha ya ndoa lakini alitoroka na kwenda kuishi porini. Anasimulia kuwa baadaye alikuja kugunduliwa na mpita njia ambaye aliamua kumrejesha nyumbani kwa wazazi wake. “Februali 6, (2024), mtu aliyemfajamu alimkuta porini akiwa amedhoofu na kumkamata na kisha kumrejesha nyumbani kwa wazazi wake,” anasema Laizer.

Laizer anasema baba mzazi wa Nanyoli, aliamua kumpigia simu mwanaume huyo na kumtaarifu kuwa mke wake alikuwa nyumbani hapo hivyo kumtaka aje kumchukua. “Baada ya kufika mwanaume huyo alimtaka binti huyo waondoke lakini alikataa ndipo alipochukua fimbo na kuanza kumshambulia mbele ya baba yake na kumjeruhi vibaya maeneo mbalimbali ya mwili wake,”anasema.

Anasema kutokana na kipigo hicho, binti huyo alipiga kelele hivyo majirani walifika nyumbani na kumkuta akiwa na hali mbaya na kuamua kumpeleka katika hospitali ya Malambo kwa ajili ya matibabu, lakini siku iliyofuata alifariki dunia. Kwa upande wake Iddy Ninga pia kutoka TAPO anasema wanataka mwili wa marehemu usizikwe hadi hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika na taarifa ya uchunguzi ikabidhiwe kwa vyombo husika vya kisheria.

Pia wamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama yakiwemo madawati ya kijinsia kutekeleza majukumu yake kikamilifu ili kuhakikisha haki inatendeka katika kushughulikia suala hilo na serikali ichukua hatuankali juu ya matukio ya aina hiyo yaliyokithiri kwa jamii za kifugaji.

Chanzo: Ngilisho News

spot_img

Latest articles

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...

Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini 📌 Apongeza utoaji wa mafunzo...

More like this

Baraza la saba la Wafanyakazi Wizara ya Nishati lakutana Dodoma

📌 Dkt. Kazungu asema Wizara itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya Kimkakati 📌 Baraza lapitisha rasimu...

Wizara ya Nishati yataja mafanikio utekelezaji majukumu 2024/25

📌 Uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 59.9 📌 Misheni 300 kuongeza upatikanaji umeme...

Gavana Tutuba: Hali ya uchumi wa Tanzania inaendelea kuimarika

Na Tatu Mohamed GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba amesema kuwa, hali...