Lissu kutohojiwa Wasafi kwamuibua Waziri Nape

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amekitaka Kituo cha Wasafi Media kupitia kipindi cha Good-Morning kufanya mahojiano na Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu huku akisisitiza kuwa hakuna kiongozi wa Serikali ambaye ana mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vya habari.

Nape ametoa kauli hiyo leo Februari 7, 2024 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma na kusisitiza kuwa kitendo kilichotokea leo kimewasikitisha na kwamba huo siyo msimamo wa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Ikumbukwe kuwa mapema leo Februari 7, 2024 Wasafi Media kupitia kipindi cha GoodMorning walitangaza kuahirisha mahojiano yao Lissu kwa kile walichoeleza kuwa ni “maagizo kutoka juu”. Hata hivyo baadaye Lissu baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Wasafi Media amesema uongozi wa kituo hicho umemwambia kuwa kuahirishwa kwa kipindi kumetokana na changamoto ya mawasiliano ya ndani.

Nape katika mkutano wake amesema Serikali tangu Rais Samia aingie madarakani amechukua hatua kubwa za kuimarisha uhuru wa Vyombo vya Habari na Demokrasia ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya sheria na kanuni za habari.

“Kitendo kilichotokea leo kimetusikitisha na maneno ya kwamba kuna maagizo kutoka juu kwenye kuingilia uhuru wa habari pia limetusikitisha, sasa nimekuka kwanza kuwathibitishia msimamo wa Rais Samia katika kuimarisha uhuru wa wanahabari na Demokrasia bado uko thabiti na uko palepale.

“Serikali yake haijafanya, haina mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vya habari. Wito wangu ni kuwaomba wanahabari tutoke kwenye hofu ambayo haina sababu, serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa wanahabari kutimiza majukumu yao.

“Hakuna kiongozi yeyote wa Serikali ambaye ana mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vyetu vya habari kutimiza majukumu yao, uhuru uko palepale, nataka kutoa wito kwa wenzetu wa Wasafi hiki kipindi walichokiahirisha wakifanye, vyombo vingine vyote vya habari wapeni uwanja sawa wanasiasa watimize majukumu yao, mtu akisemwa wa upande wa pili apewe nafasi ya kujieleza,” amesema Nape.

spot_img

Latest articles

Dkt Biteko: Serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya Afya

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeahidi kuendelea...

THRDC yashauri kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)...

Sh. Bilioni 30 zaidhinishwa kujenga Barabara zilizoathiriwa na mvua

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha...

Ewura yazitaka kampuni za gesi kuongeza mawakala, kudhibiti uchakachuaji wa gesi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za nishati na...

More like this

Dkt Biteko: Serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya Afya

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru Na Mwandishi Wetu SERIKALI imeahidi kuendelea...

THRDC yashauri kuitishwa mkutano wa kitaifa wa maridhiano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)...

Sh. Bilioni 30 zaidhinishwa kujenga Barabara zilizoathiriwa na mvua

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imepanga kutumia kiasi cha...