Yanga kufanya sherehe  Mbeya, ikicheza na Prisons

Na Winfrida Mtoi

Klabu ya Yanga imepanga kufanya sherehe ya  kuadhimisha  miaka 89 tangu kuzaliwa kwake  Februari 11,2024, jijini Mbeya siku ambayo itakutana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 5, 2024 jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ally Kamwe amesema tayari matukio mbalimbali kuelekea kilele cha maadhimisho hayo yameanza na kesho wanatarajia kuingia mkataba na hospitali kubwa nchini.

Amesema lengo la kuingia mkataba na hospitali hiyo ambayo hakuitaja jina ni kuweza kuwasaidia mashabiki wao katika suala la afya.

“Kesho Yanga inakwenda kusaini mkataba na hospitali kubwa sana duniani, ikiwa na lengo la kumnufaisha shabiki wetu kwenye masuala yanayohusu afya yao. Pia Jumatano tunazindua upya ofisi yetu pale Jangwani.

“Mkoa wa Mbeya umepata bahati ya kusheherekea ‘anniversary’ ya mabingwa wa kihistoria. Naomba mashabiki wote wa Yanga popote walipo wakaweke kambi Mbeya na tutazindua na nyimbo mbili kutoka kwa wasanii wakubwa,” amesema Kamwe.

spot_img

Latest articles

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

Waziri Ndejembi afungua kikao cha 55 cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Tanesco Dodoma

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, leo tarehe 22 Januari, 2026 amefungua...

More like this