Wachezaji 21 waitwa kikosini Tembo Warriors

Na Winfrida Mtoi

Jumla ya wachezaji  21 wameitwa kuunda  timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ kujiandaa na   mashindano ya Afrika  yatakayofanyika Aprili 14- 29,2024 nchini Misri

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 22, 2024, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka kwa watu wenye ulemavu Tanzania (TAFF),  Athumani Lubandame, amesema tayari timu hiyo imeanza mazoezi.

” Sasa timu imeanza mazoezi rasmi ambayo yanafanyika Uwanja wa Uhuru, huku  tukiwa tunasubiri maelekezo ya Serikali kuingia kambi ya pamoja baadaye,” amesema Lubandame.

Kwa upande wake, Meneja wa timu hiyo, Zaharani Mwenyemti ,amesema lengo lao ni kufika fainali ya michuano hiyo.

Amesema wanataka kwenda   kutetea nafasi ya nne Afrika iliyowafanya  wafuzu Kombe la Dunia ambapo  waliishia hatua ya robo fainali.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Salvatory Edward , ametaja majina ya wachezaji walioitwa  kuwa ni  Bashara Alombile, Ally Juma Abdallah, Hassan Vuai Ameri, Abdulkarim Amin Khalifa, Shadrack  Hebron Sembele, Richard Fredy Swai, Ramadhan Ally Chomero.

Wengine ni Juma Mohamed Kidevu, Salimu Rashid Bakari, Steven Manumba Antony, Habibu Saidi, Salehe Mwipi, Khalfan Athumani,Emmanuel Nakala, Adamu Hassan, Lifati Anasi,Rojas Kadora, Julius Ngume, Kassimu Mohamed, Frank Ngairo na Wistin Sango.

spot_img

Latest articles

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...

Rais Samia kuzindua Dira ya Taifa ya 2050

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa...

More like this

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...