Mwakinyo atamba yuko fiti asilimia 98 kupanda ulingoni Zanzibar

Na Winfrida Mtoi

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya pambano lake dhidi ya Mbiya Kanku litakalofanyika Januari 27, 2024, bondia wa Hassan Mwakinyo amesema amekamilisha maandalizi kwa asilimia 98 kilichobaki ni kupima uzito pekee.

Mwakinyo na Kanku raia wa DR Congo wanatarajiwa kupanda ulingoni katika pambano la ubingwa wa WBO Afrika litakalopigwa Amani Complex Indoor Arena, Zanzibar.

Mwakinyo amesema amejiandaa kila idara, hivyo mpizani hata akimjia kwa mtindo gani yupo tayari kupambana naye, kwani mikono ndiyo itaongea ulingoni.

Bondia huyo mwenye jina kubwa nchini, amewatoa hofu mashabiki wa masumbwi visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuwa siku hiyo ataonesha burudani ya kuvutia ya ngumi.

Mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo, Hussein Itaba dhidi ya Juma Misumari wa Morogoro, Bakari H.Bakari na Seleman Hamad, Masoud Khatibu atazichapa na Yahaya Khamis, huku mwanadada Zulfa Iddi akivaana na Debora Mwenda.

spot_img

Latest articles

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...

SGR yapata ajali, TRC yataja chanzo

Na Mwandishi Wetu Treni ya Mwendokasi (SGR) imeacha njia yake na kupata ajali katika eneo...

More like this