Sisi ndiyo tuliomrudisha Makonda. Tusiishie kulaumu, tujitafakari

KUNA jina moja tu sasa masikioni mwa Watanzania wanaofuatilia siasa. Paul Christian Makonda.

Huyu ndiye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo.

Makonda wa leo, kwa madaraka na mamlaka yake haya, ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM. Vikao vikuu vitatu vya maamuzi ya kisiasa na mwelekeo wa kiserikali kitaifa.

Makonda huyu wa leo ni zao la siasa za ndani na nje ya CCM katika siku na miaka ya hivi karibuni.

Ndani ya CCM, simulizi za chini ya uvungu na maneno yasiyosikika yanasema, viongozi wakuu na wa juu wastaafu, viongozi waandamizi na watu wenye ushawishi ambao Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliwafungulia masikio na moyo wa usikivu kwa sababu wanazojua wao vyema, wanamfitini chini kwa chini.

Paul Makonda Picha|Mtandao.

Nje ya CCM, Rais na Mwenyekiti wa CCM aliyenyoosha mikono ya kusaka maridhiano na makundi mbalimbali ya kisiasa na kijamii kwa kiwango cha kujitoa kulipa hadi fidia kwa walioumizwa zama za Serikali ya Awamu ya Tano ya John Pombe Magufuli (JPM) amegeukwa na wale wale aliojitoa mhanga kuwapigania na kuwarejeshea haki zao.

Kundi jingine ni la viongozi wa dini hususan maaskofu 37 wa TEC waliojipambanua pia ‘kumkabili’ Samia wakiwa nyuma ya pazia la DP World.

Nje ya makundi hayo liko kundi la Sukuma Gang au Magufuli Yekkha. Hili lina watu ndani na nje ya vyama vya siasa, hili kundi ambalo Samia alifikiri lingemwelewa kwa kuonyesha kwa kauli na matendo kwamba angeenzi kazi za shujaa wao limempa mgongo na limeungana na akina Slaa, Mwabukusi, Mbatia na wengine kumsakama Samia.

Ni hivi, baada ya kumfikisha hapo Samia akaona hili lisiwe shida, akampandisha chati Dotto Biteko, akampa cheo, Alexander Pastory Mnyeti na mwisho akamwinua, Paul Christian Makonda.

Watatu hao ni mkakati mahususi wa Samia kukabiliana na kimbunga ambacho kilikuwa kikitengenezwa na makundi hayo manne.

Kundi baya na la hatari zaidi kwa Samia ni la viongozi wakuu wastaafu wachimvi ambao wako hivyo si kwa sababu yoyote ile bali wametokea tu kuwa watu wa husuda, wanaodai zaidi ya fadhila, wasioridhika kwa lolote, walipa mabaya kwa mema na watu wasio na shukrani.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kundi hili halikubaliani na maridhiano ya Samia, linakerwa na Uzanzibari wake na lina hisia hasi kwa jinsia yake na mwisho linaonyesha dharau kwa Rais na pengine kwa mamlaka yake. Katika kundi hilo wako watu tunaowapenda na kuwaheshimu.

Haya yote yamechagiza kwa kiwango kikubwa kuibuliwa la Paul Makonda kwa mfano wa yale makombora yasiyo na ubinadamu au utu yanayovurumishwa na Israel dhidi ya Palestina kwa sababu tu ya makosa ya kimkakati ya kundi la Hamas.

Mazingira yamemlazimisha Rais Samia kumleta ‘mwendawazimu’ katika kiringe cha siasa kwa namna ile ile ambayo Mwalimu alilazimika kumleta Edward Moringe Sokoine na Mzee Mwinyi akampandisha kimamlaka Augustine Lyatonga Mrema.

Ni sababu kama hizo ambazo JK alizitumia kumbeba Nape Nnauye ambaye naye akishirikiana na akina Daniel Chongolo wakati wa Abdulrahman Kinana wakaja na akina Makonda.

Ni kwa namna hiyo hiyo JPM alikuja na wendawazimu wake kama Cyprian Musiba na kwa sehemu akina Bashiru Ali, Humphrey Polepole na Paul Makonda.

Historia hujirudia na mara nyingi hurudi ikiwa imefanyiwa ukarabati.

Mazingira ndiyo yamemleta Makonda. Wako wa kijiuliza, wako wa kulaumu na wako pia wanaopaswa kujilaumu wao wenyewe. Sisi wengine tunapaswa kujifunza na kutafakari.

Kila mmoja apime kwa nafsi yake mchango wake katika kumrejesha Makonda kiringine. Imeandikwa Mpende Adui yako. Imeandikwa pia Mpende jirani yako kama nafsi yako. Nampenda Paul Christian Makonda.

spot_img

Latest articles

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...

Watu wawili wafariki, 16 wajeruhiwa katika ajali ya basi Songwe

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Watu wawili wamefariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya...

More like this

Soma Ripoti ya UHIFADHI WA UHAI: UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NDANI YA SEKTA YA UHIFADHI TANZANIA

Na Mwandishi Wetu, Media Brains Utafiti mpya umebaini kwamba mamlaka za serikali zimekuwa kichocheo kikuu...

RAIS DKT. SAMIA ATOA MAAGIZO KWA BASHE, NFRA KUNUNUA MAHINDI KWA WAKULIMA TSH 700 KWA KILO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassanamemuagiza Waziri wa Kilimo...

Upi upepo unaoweza kufika Tanzania,wa Wiliam Ruto au Paul Kagame?

KUNA upepo wa aina mbili unavuma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mmoja...