Chuo Kikuu Mzumbe kuandaa wataalam miradi ya kimkakati

Mwandishi Wetu, Media Brains

Chuo Kikuu Mzumbe (MU), kimeweka mikakati ya kuandaa wataalam watakaosimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme katika Bonde la Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge), ujenzi wa bomba la gesi kutoka Tanzania hadi Uganda na mingine.

Akizungumza Dar es Salaam Julai 18,2023 kwenye Maonesho ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yanayoratibiwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mratibu wa Udahili, Dk. Michael Mangula, amesema miradi mingi imekuwa si endelevu hivyo kupitia programu hizo wataalamu watapatikana wa kuisimamia.

Kulingana na Dk. Mangula, chuo kimeanzisha programu tatu mpya ambazo ni Shahada ya Utawala wa Umma katika Maendeleo ya Vijana na Uongozi kwa lengo la kaandaa wataalam watakaosimamia maendeleo ya vijana.

Nyingine ni Shahada ya kwanza ya Mfumo wa Afya katika ufuatiliaji wa tathmini ambayo inawaandaa wataalamu wanaosimamia miradi kwenye sekta ya afya na Shahada ya Usimamizi wa Mazingira inayowaanda wataalamu kusimamia shughuli za mazingira.

“Kwenye maonesho haya tunawaelimisha wazazi na wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha nne, sita na diploma. Tumefungua dirisha la udahili kuanzia ngazi ya cheti, diploma, shahada za awali, shahada za umahiri na shahada za Uzamivu.

“Watanzania watembelee banda letu hapa Mnazi Mmoja kupata udahili wa moja kwa moja. Wanapofika kwanza tunawaelimisha juu ya programu zinazopatikana chuoni kwetu na sifa zinatotakiwa ili mwanafunzi aweze kujiunga,” amesema Dk. Mangula.

Amesema chuo hicho kinatoa mafunzo ya muda mrefu kwenye maeneo mbalimbali ya ubobezi katika sheria, utawala na menejimenti, biashara, ujasiriamali, uhasibu na fedha, uchumi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Maeneo mengine ni takwimu tumizi, ualimu, usimamizi wa shughuli za uzalishaji viwandani, kuandaa wahandisi katika usimamizi wa uzalishaji kwenye viwanda.

spot_img

Latest articles

BANDA LA DAWASA LAVUTIA USHIRIKI VIONGOZI NA WAGENI COP12

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA)...

KABUDI: VYAMA VYA SIASA VIENDELEE KUJENGA UTAMADUNI WA MAZUNGUMZO

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu,...

MWABUKUSI ATAKA BARAZA LA VYAMA KUWA NA KAMATI YA MAKOSA YA KISIASA

Na Tatu Mohamed RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amelishauri Baraza...

RASILIMALI ZA BAHARI ZATOA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UCHUMI WA BULUU

Na Tatu Mohamed TANZANIA na nchi nyingine za Bahari ya Hindi Magharibi zimetakiwa kutumia...

More like this