Warning: Array to string conversion in /home/themedia/domains/themediabrains.com/public_html/wp-includes/shortcodes.php on line 434
Array

Wakurugenzi wa mashirika watahadharishwa

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Msajili wa Hazina nchini, Nehemia Mchechu, ametangaza uamuzi mgumu kwa viongozi wa Mashirika ya Umma ambayo yatashindwa kujiendesha kwa mujibu wa sheria.

Amesema katika mkakati wa sasa wa Ofisi ya Msajili ni kuhakikisha kila kiongozi atayeteuliwa na mamlaka za uteuzi ni katika kuendesha shirika lazima afanyiwe tathmini ndani ya miaka miwili au mitatu na pindi anaposhindwa atapisha watu wengine.

Hatua hiyo inakuja baada ya hivi karibuni, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kumwagiza Msajili wa Hazina kuyafuta mashika ya umma ambayo yameshindwa kujiendesha na yamekuwa yakiitia hasara Serikali licha ya kupewa fedha za kujiendesha kwa mujibu wa sheria lakini bado wameshindwa kutoa gawio kwa serikali.

Akizungumza leo Julai 13, 2023 Jijini Dar es Salaam na Wahariri wa vyombo vya habari, Mchechu amesema kwa sasa ofisi ya msajili inasimamia mashirika ya umma 301 kutoka 248 ya awali ingawa kwa baada ya muda mfupi yapo baadhi ya mashirika yataunganishwa hasa baada ya kukamilika kwa kazi ya kupitia muundo wake.

“Juzi sote tulimsikia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akiagiza tuvunje mashika ambayo hayafanyi vizuri licha ya kupewa uwezo wa kujiendesha na serikali. Lakini kutokana na sasa kutokana na muundo tumeweza kuanza mapya na mengine tutayaunganisha.

“Mashirika yote nchini hasa yale ya umma yanapaswa kuwa ‘active’ (imara) wakati wote na kutoa mchango kwa Serikali. Kwani tunajua yapo baadhi ya mashika yanategemea mchango wa serikali ili yaweze kujiendesha wakati yanatakiwa kujiendesha wenyewe baada ya kupewa mtaji.

“Katika siku 100 za kwanza tumeweza kufanikiwa masuala kadhaa katika mashirika yetu. Ukiangalia makampuni binafsi yanafanya vizuri ikiwamo kampuni kama za Bakhressa, tena huyu ni mtu binafsi ambaye anazalisha kwa wingi na kwa faida kubwa. Au Vodacom inafanya vizuri huku TTCL ikishindwa? kwa nini ya kwetu (Serikali) hayafanyi vizuri licha kuwezeshwa kwa kupewa ruzuku na mitaji,” amehoji Mchechu

Msajili huyo wa Hazina, amesema inataka kuhuisha mashirika kwa mfumo wa Holding Company (Kampuni Hodhi) ikiwamo kuyaangalia kwa jicho cha biashara kwa kila shirika la umma kwani kutofanya hivyo tija itakosekana.

Amesema katika kusimamia mkakati huo kuanzia sasa ofisi yake inataka mashirka yote yawe wazi kwa umma kwa kueleza shughuli zake kupitia vyombo vya habari badala ya kusubiri jicho la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pekee.

“Tunataka kuwepo na ushirikiano kati ya mashirika, Wahariri na Waandishi wa Habari hasa yale ambayo yapo kwa Msajili wa Hazina ikiwamo kutoa taarifa zao kwa mashirika yote ili umma uweze kujua kinachoendelea. Leo ni kuwapa nafasi watanzania badala ya kusubiri mapungufu aliyobaini CAG mashirika yaseme yenyewe na umma ujue kwa uwazi na hii ni sehemu ya mabadiliko ambayo tunakwenda nayo kwa sasa.

“Nchi yetu bado inategemea kilimo na kwa Serikali tumeipa uwezo Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ambaye ni muhusika mkubwa katika kusimamia hili na leo tutaanza nayo kama utaratibu wetu, tunajua wahariri na waandishi mna nafasi kubwa katika kutueleza changamoto zetu,” amesema Mchechu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TADB, Frank Nyabudenge amesema benki hiyo ina malengo ya kufanya mapunduzi makubwa kwenye sekta ya kilimo ndio maana wanatoa mitaji kwa wakulima na kuongeza kwa sasa benki hiyo inazidi kupasua anga na kuna ongezeko kubwa la mikopo katika Serikali ya Awamu ya Sita.

”Idadi ya mikopo imekuwa ikipanda tulikuwa na mikopo  Sh bilioni 110, ikipanda hadi Sh bilioni 152 ikafika Sh bilioni 262, na hadi kufikia Juni 30, 2023 tulikuwa na  jumla ya mikopo Sh bilioni 317 na tunaamini hadi kufikia mwezi Desemba mwaka huu itaongezeka zaidi,” amesema Nyabudenge.

Mkurugenzi huyo amesema lengo lao ni kutanua wigo wa benki hiyo pamoja na kubadili mfumo wa kilimo Tanzania, lakini pia kuchagiza taasisi nyingine za kifedha kutoa mitaji kwa wakulima.

spot_img

Latest articles

Kikwete mgeni rasmi kongamano la PBA kesho

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikkwete anatarajiwa kuwa...

Mwanza journos sharpen skills for upcoming elections

By Our Correspondent, Mwanza The Resident Representative of the non-governmental organization Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung nchini, Peter Koch,...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

Na Mwandishi Wetu, Mwanza MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung...

More like this

Kikwete mgeni rasmi kongamano la PBA kesho

Na Mwandishi Wetu RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikkwete anatarajiwa kuwa...

Mwanza journos sharpen skills for upcoming elections

By Our Correspondent, Mwanza The Resident Representative of the non-governmental organization Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Wanahabari Mwanza wafundwa kuhusu Sheria za Uchaguzi, maadili

MWAKILISHI Mkazi wa shirika lisilo la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung nchini, Peter Koch,...