Bodi ya DAWASA yasisitiza kukamilika kwa wakati ufungaji pampu mpya za maji

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhandisi Romanus Mwang’ingo, imekagua zoezi la ufungaji wa pampu mpya za kusukuma maji ghafi katika Mtambo wa Kuzalisha Maji wa Ruvu Juu uliopo Mlandizi, mkoani Pwani na kusisitiza ukamilishaji wake kwa wakati.

‎‎Pampu hizo, zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16, zinatarajiwa kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa maji, na kuboresha huduma kwa zaidi ya wakazi milioni saba wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

‎‎Katika ziara hiyo, Bodi pia ilipokea taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kudhibiti upotevu wa maji katika maeneo ya Mlandizi na Kibaha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa DAWASA wa kupunguza upotevu wa maji na kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi.‎‎

Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mhandisi Mwang’ingo aliwataka watumishi wanaosimamia mradi huo kuendelea kufanya kazi kwa weledi, kujituma na kuhakikisha ufungaji wa pampu unakamilika kwa wakati.‎‎

“Niendelee kuwatia moyo watumishi mnaoendelea na kazi hii kuifanya kwa weledi na kuikamilisha kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora na endelevu ya majisafi na salama. Hili ni jukumu letu sote,” amesema Mhandisi Mwang’ingo.

‎‎Amesisitiza kuwa kukamilika kwa mradi huo kwa wakati kutakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha upatikanaji wa maji na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi wa Dar es Salaam na Pwani.‎‎

DAWASA inaendelea kutekeleza maboresho mbalimbali ya miundombinu ya uzalishaji na usambazaji wa maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya majisafi na salama kwa uhakika na kwa viwango vinavyokidhi mahitaji yanayoongezeka.‎‎

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this