JAB YASOGEZA HUDUMA ZA ITHIBATI KARIBU NA WAANDISHI DODOMA

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imeanza kutoa huduma mbalimbali za ithibati katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma na kutatua changamoto zinazowakabili waandishi wa habari.

Kupitia banda la Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, maafisa wa JAB wanaendelea kuhudumia waandishi wa habari na wananchi kwa kutoa elimu kuhusu mchakato wa ithibati, kusaidia usajili kwa waombaji waliokwama kutumia mfumo wa TAI HABARI pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu Sheria ya Huduma za Habari.

Aidha, waandishi wa habari ambao maombi yao yameidhinishwa wanaendelea kupokea vitambulisho vyao vya ithibati katika maonesho hayo, hatua inayowawezesha kupata huduma kwa haraka bila kulazimika kufika katika ofisi za JAB.

Maafisa wa JAB, Mawazo Kibamba na Happiness Chindiye, wamekuwa wakitoa huduma hizo moja kwa moja kwa wadau wanaotembelea banda hilo, sambamba na kupokea maoni, maswali na changamoto zinazohusu utekelezaji wa mfumo wa ithibati nchini.

Huduma hizo ni sehemu ya jitihada za JAB za kuimarisha uwajibikaji, kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi kwa kuhakikisha waandishi wa habari wanapata msaada kwa wakati, sambamba na kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu isemayo “Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”

spot_img

Latest articles

Wadau wavutiwa elimu ya vipimo maadhimisho wiki ya utumishi wa umma

Na Mwandishi Wetu WADAU mbalimbali waliotembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika siku ya...

Tanesco yakamilisha miradi ya kuimarisha upatikanaji wa umeme Dodoma

📌 Itanufaisha wilaya za Kongwa,Gairo, Mpwapwa, na Chamwino 📌 Waziri Ndejembi azindua Kituo cha...

Taasisi za Umma Kukabidhi gawio Ikulu Juni 30 Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina imetangaza siku ya Gawio 2026 itafanyika...

More like this