Dawasa yatoa elimu Uhifadhi wa maji katika wiki ya mazingira

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, yakiwa na kauli mbiu isemayo: “Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania.”

Maadhimisho hayo yanayofanyika kuanzia Juni 1 hadi 5 kila mwaka yamewakutanisha wadau kutoka sekta za umma na binafsi kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za taifa na kujadili mikakati ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo kitaifa, Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa mazingira katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Amesema juhudi za uhifadhi wa mazingira zinapaswa kupewa kipaumbele kupitia upandaji miti kwa kiwango kikubwa, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha biashara ya kaboni na utekelezaji wa miradi ya kijani.

Katika maadhimisho hayo, DAWASA inashiriki kupitia banda la Wizara ya Maji na Taasisi zake, ambapo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma za majisafi na usafi wa mazingira, umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji, pamoja na miradi na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi sambamba na umuhimu wa Wananchi katika kulinda vyanzo vya maji kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this