‎Msigwa: Bwawa la Kidunda ni mradi wa kimkakati kwa Maji, Kilimo na Nishati

Na Mwandishi Wetu

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameipongeza Wizara ya Maji kwa usimamizi madhubuti wa ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda, akieleza kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati Nchini inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya maji, kilimo, nishati na uhifadhi wa mazingira nchini.‎‎

Msigwa, ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi wa Bwawa la Kidunda mkoani Morogoro, ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 50.3.‎‎

Amesema kukamilika kwa bwawa hilo kutakuwa suluhisho la muda mrefu kwa changamoto za upungufu wa maji kwa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huku likiimarisha uwezo wa mitambo ya kuzalisha maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini inayosimamiwa na DAWASA.‎‎

“Baada ya kusuasua kwa muda mrefu tangu mwaka 1961, tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuidhinisha Shilingi bilioni 336 zilizowezesha kuanza kwa mradi huu mkubwa na wa kihistoria mara baada ya kuingia madarakani. Mradi huu utanufaisha zaidi ya wananchi takriban milioni saba wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani,” amesema Msigwa.‎‎

Ameeleza kuwa mbali na kuongeza uhakika wa maji kwa wananchi, mradi huo utakuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta za kilimo, uvuvi na uzalishaji wa nishati ya umeme wa megawati 20.

‎‎Msigwa pia amefafanua Bwawa la Kidunda limezingatia masuala ya uhifadhi wa mazingira na kwamba hofu zilizokuwapo awali kuhusu athari zake si za kweli.‎‎ “Maji yatakayokusanywa hapa ni lita bilioni 190.

Kati ya hizo, lita bilioni mbili pekee ndizo zitakazotumika kwa siku. Zaidi ya lita milioni 600 zitaelekezwa kwenye mitambo ya DAWASA, lita milioni 400 zitahudumia mashamba ya sukari ya Mkulazi, huku zaidi ya lita milioni 900 zikiendelea kuhifadhi na kulinda ikolojia ya Mto Ruvu,” amesisitiza.‎‎

Kwa upande wake, Msimamizi wa Mradi kutoka DAWASA, Mhandisi Christian Christopher, amesema ujenzi wa bwawa hilo unaendelea kwa kasi na umefikia asilimia 50, huku matarajio yakiwa ni kuukamilisha ifikapo Desemba 2026.

‎‎Amesema kazi mbalimbali zinaendelea katika maeneo tofauti ya mradi ili kuhakikisha utekelezaji wake unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.‎‎

Bwawa la Kidunda linatajwa kuwa miongoni mwa miradi muhimu ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa maji wa uhakika kwa wananchi, kuimarisha shughuli za uzalishaji mali na kuchochea maendeleo endelevu ya taifa.‎‎

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...