Watu 1,066 wapoteza maisha ajali za barabarani

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi amesema jumla ya Watu 1,066 wamepoteza maisha kwa ajali za barabarani katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 ikilinganishwa na Watu 1,275 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho cha mwaka 2025/2026.

Katambi ameyasema hayo leo Mei 25, 2026 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2026/27.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa, matukio ya usalama barabarani yaliyotolewa taarifa katika vituo vya polisi nchini yamepungua kutoka 1,322 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Aprili 2025 na kufikia 1,233 katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2025/26.

“Katika matukio hayo, jumla ya watu 1,066 walipoteza maisha ikilinganishwa na watu 1,275 waliopoteza maisha katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2024/25 ikiwa ni upungufu wa asilimia 16.4. Vilevile, watu 1,869 walijeruhiwa ikilinganishwa na watu 2,278 waliojeruhiwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2024/25 ikiwa ni upungufu wa asilimia 18. 42.

Amesema katika mwaka 2026/27 wizara kupitia Jeshi la Polisi itaendelea na mikakati ya kusimamia ipasavyo sheria ya usalama barabarani kwa kufanya doria na kuchukua hatua stahiki kwa wanaokiuka sheria hiyo.

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this