Nusu fainali Kombe la shirikisho, Chama atakuwa Arusha, Diarra Mwanza  

Na Winfrida Mtoi

MCHEZO wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Coastal Union unatarajiwa kuchezwa Juni 20, 2026 katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, wakati Yanga itakutana na Azam FC  nusu fainali ya pili, dimba la CCM Kirumba, jijini Mwanza, Juni 21, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, Mei 18, 2026 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika kwa michezo ya robo fainali.

Simba imetinga nusu fainali baada ya jana Mei 17, 2026 kuichapa TRA united mabao 4-0 katika  mchezo uliopigwa KMC Complex, jijini Dar es Salaam. Yanga iliifunga JKT Tanzania mabao 2-0 Uwanja wa Maj. Gen. Isamuhyo.

Azam FC iliichapa Mashujaa bao 1-0  jana katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, huku Coastal Union ikitinga nusu fainali kwa kuiondosha  Singida Bs kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kutoka suluhu ndani ya dakika 90, kwenye dimba la Mkwakwani Tanga.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this