Didier Drogba atikisa Bunge la Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Shangwe​  zimetawala  katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma leo Mei 4, 2026,   baada ya gwiji wa soka duniani na nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ivory Coast na mchezaji wa Chelsea,  Didier Drogba kutambulishwa mbele ya  wabunge na wageni waalikwa.

​Drogba, ambaye aliwasili nchini jana kwa mwaliko rasmi wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Paul Makonda, amepata mapokezi ya kipekee na kuwa kivutio bungeni.

​Lengo la ziara ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 48, ambaye miongoni mwa wachezaji bora walioweka alama katika soka  barani Afrika na duniani,  ni kuunga mkono jitihada za kukuza michezo na utalii nchini.

Drogba anakumbukwa kama mshambuliaji mwenye nguvu na ushawishi mkubwa, hasa katika klabu ya Chelsea ambako alicheza kwa mafanikio makubwa.

​Klabu nyingine alizowahi kuchezea nyota huyo ni ​​Olympique Marseille (Ufaransa), ​Shanghai Shenhua (China), ​Galatasaray (Uturuki), ​Montreal Impact (Canada/MLS) na ​Phoenix Rising (Marekani)

spot_img

Latest articles

Rais Ruto awasili nchini

Na Mwandishi Wetu Rais wa Kenya, Dk. William Ruto amewasili nchini leo kwa ziara ya...

Makonda aomba sh.525.32 bilioni, maandalizi AFCON yafikia pazuri

 Na Mwandishi Wetu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda ameomba sh. 525.32...

Waogeleaji 19 wapaa Argeria, kuiwakilisha Tanzania mchuano ya Afrika

Na Winfrida Mtoi JUMLA ya waogeleaji 19 wamekabidhiwa bendera Mei 2, 2026 kwenda kuiwakilisha Tanzania...

TTB yaeleza Utalii wa michezo unavyochangia uchumi wa jamii

Na Mwandishi Wetu, Njombe BODI ya Utalii Tanzania (TTB), imesema utalii wa...

More like this