DC Mkude akabidhi vyombo vya usafiri Tanesco Mkoa wa Arusha kuimarisha utoaji huduma

📌 Ni katika muendelezo wa mkakati wa TANESCO wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

📌 Awataka kutumia vyombo hivyo kwa kazi husika za TANESCO

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MKUU wa Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha, Joseph Mkude amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO Mkoa wa Arusha ili kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali za Shirika kwa wananchi.

Akizungumza tarehe 13, Aprili 2026 wakati wa hafla ya kukakabidhi vitendea kazi hivyo iliyofanyika katika Ofisi za TANESCO Mkoa wa Arusha amesema hatua hiyo ya kukabidhi vitendea kazi hivyo ni hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za umeme wa uhakika bila vikwazo vyoyote.

Amesema vitendea kazi hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wa TANESCO katika wilaya za Mkoa wa Arusha na kuwawezesha kutatua changamoto za wateja kwa wakati kwani Magari pamoja na Bajaji zitawawezesha kuyafikia maeno mengi zaidi ili kufikisha huduma ya umeme.

Amewataka Watumishi wa TANESCO Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanatumia vyema vitendea kazi hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na Shirika na wala sio kwa matumizi yao binafisi ambayo hayana faida wala mchango wowote kwa Shirika hasa katika kutoa huduma kwa wananchi.

“Haya Magari tuliyopatiwa katika Mkoa wetu yanakwenda kugawiwa katika kila wilaya naomba yakatumike ipasavyo kwa malengo yaliyokusudiwa, tusitumie Magari haya kwa mambo yetu binafsi yasiyo na tija katika kutoa huduma kwa wananchi”.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma za Usalama TANESCO, Lenin Kiobya amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliwezesha kununuliwa kwa Magari Makubwa na Madogo zaidi ya 500 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kiobya amesema kati ya Magari hayo zaidi ya 500, Malori ya ukubwa mbalimbali ikiwemo tani 10 na tani 7 yapo 215 ambayo yanakwenda kuwa msaada Mkubwa zaidi katika huduma za matengenezo ya umeme kwa wakati hali itakayochangia kuongeza ufanisi wa kazi ndani ya Shirika.

Aidha, amesema kwa Mwaka wa Fedha ujao 2026/2027 Serikali imetenga zaidi ya bilioni 200 ili kununua vitendea kazi hivyo lengo likiwa ni kumaliza kabisa upungufu wa vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO katika maeneo yote nchini.

“Serikali iliwezesha TANESCO kuweza kunua Magari 556 kwa mwaka huu wa fedha 2025/2026 ili kurahisisha utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi, na kwa mwaka ujao wa fedha 2026/ 2027 Serikali imetenga zaidi ya bilioni 200 ili kununua vitendea kazi hivyo lengo likiwa ni kumaliza kabisa upungufu wa vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO” amesema.

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha Mhandisi Kisika Kisika amesema TANESCO katika Mkoa huo wamepokea vitendea kazi mbalimbali ikiwemo Magari makubwa 2, Gari aina ya Landcruser (4), Bajaji moja (1) vitakavyokwenda kuboresha zaidi huduma kwa wateja katika Mkoa huo.

“Tunaishukuru Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutupatia vitendea kazi hivi ambavyo kwa sasa tunakwenda kuvitumia kufikisha huduma kwa wananchi kwa haraka zaidi.

spot_img

Latest articles

Rais Mwinyi akagua Mji wa AFCON Fumba

Na Mwandishi WetuRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sowah apigwa faini nzito  kwa utovu wa nidhamu, ashushwa U-20

Na Winfrida Mtoi UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka wazi hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa...

Waziri Mavunde aelekeza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji Busulwangili-Kahama – Kahama

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa...

DCEA yakamata Kilo 101.2 za Mirungi ndani ya Basi la Abood, watano mbaroni

Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata...

More like this

Rais Mwinyi akagua Mji wa AFCON Fumba

Na Mwandishi WetuRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sowah apigwa faini nzito  kwa utovu wa nidhamu, ashushwa U-20

Na Winfrida Mtoi UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka wazi hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa...

Waziri Mavunde aelekeza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji Busulwangili-Kahama – Kahama

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa...