Waliotafuna fedha za AMCOS Mbozi waanza ‘kuzitapika

SHILINGI milioni 170 ambazo ni sehemu ya mamilioni ya fedha zilizobainika kutafunwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika (AMCOS) vinane katika wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, zimerejeshwa.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema leo bungeni Dodoma kuwa fedha hizo ni sehemu ya Sh. Milioni 294 ambazo serikali inaendelea kupambana ili kuzirejesha kwa wakulima.

Akijibu swali la mbunge wa Mbozi, George Mwenisongole, Bashe amesema mpaka sasa vyama vya ushirika 20 vimechunguzwa na vinane (8) vimebainika kufanya ubadhirifu na wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Mbunge Mwenisongole alitaka kufahamu lini serikali itaanza uchunguzi kwa vyama vya (AMCOS) ambavyo awali havikufanyiwa uchunguzi dhidi ya tuhuma za ubadhirifu kwa wakulima.

Bashe amesema unaofanywa kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika utazifikia AMCOS 98 za wilayani Mbozi na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2024.

spot_img

Latest articles

Azam yamrejesha Manula

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Azam imemrejesha golikipa wao wa zamani, Aishi Manula akitokea Simba...

Fountain Gate FC yakwepa kushuka daraja

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao...

Tyson wa Bongo afunga mtaa 

Na  Winfrida  Mtoi Bondia wa ngumi za kulipwa Hassan Ndonga maarufu Tyson wa Bongo amefunga  Mtaa wa Banda Mabibo,...

Rais Samia kuzindua Dira ya Taifa ya 2050

Na Mwandishi Wetu Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa...

More like this