Naibu Waziri wa Nishati akabidhi vitendea kazi Kwa Tanesco Mkoa wa Shinyanga

📌Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi

📌Awasihi wananchi kutumia nishati safi umeme kupikia

Na Mwandishi Wetu, Kahama

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kutatua changamoto zao kwa haraka.

Akizungumza leo tarehe 27, Machi 2026 wakati wa hafla ya kukakabidhi vitendea kazi hivyo iliyofanyika katika Manispaa ya Kahama Mkaoni Shinyaga Salome amesema hatua hiyo ya kukabidhi vitendea kazi hivyo ni kuyaishi maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Umeme wa uhakika.

Amesema vitendea kazi hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na kuwawezesha kutatua changamoto za wateja kwa wakati.

“Kupitia vyombo hivi vya usafiri vitakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika kumfikia mteja kwa haraka na kumhudumia, niwaombe mvitumie kutatua changamoto zao kwa wakati “ amesema Salome.

Aidha Salome ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa Manispaa ya Kahama kuchangamkia matumizi ya Nishati safi ya umeme kupikia kwani Nishati ya umeme ni nafuu salama na rafiki kwa mazingira.

“Niwaombe wakina mama wa Kahama tuchangamkie matumizi ya nishati safi ya kupikia ya umeme, TANESCO wameleta majiko hapa unapika kwa urahisi na haraka zaidi” amesema.

Hata hivyo, Salome amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme TANESCO inaendelea kwa kasi kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Manispaa ya Kahama kutokana na kuendelea kukua kwa Mji huo ambapo mpaka sasa tayari zaidi ya Shilingi milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kujenga laini mpya ya umeme itakayo wahudumia wakazi wa Manispaa ya Kahama.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Benson Mbigili amesema wamepokea vitendea kazi mbalimbali ikiwemo Magari manne (4), Bajaji moja (1) pamoja na Pikipiki nne (4). Mha. Benson ameipongeza Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kwa kuwezesha vitendea kazi hivyo ambavyo kwa sasa wanakwenda kuvitumia kufikisha huduma kwa wananchi kwa haraka zaidi.

Amesema kupitia Magari hayo sasa yatawasaidia kuwafikia wateja wapya katika maeneo yote hasa yale korofi ambapo kabla ya Magari hayo ilikuwa changamoto kuwafikia na kuwaahidi wananchi kuendelea kutoa huduma bora na ya uhakika kila wakati.

“Tunaishukuru Serikali kupitia Shirika la umeme Tanzania TANESCO kwa kutupa vitendea kazi hivi ambavyo kwa sasa tunakwenda kuvitumia kufikisha huduma kwa wananchi kwa haraka zaidi,” amesema.

Aidha amesema TANESCO Mkoa wa Shinyanga inaendelea kwa kasi kubwa kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia kwa umeme ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa kutumia nishati hiyo kupikia.

spot_img

Latest articles

NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa...

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

Dkt. Mataragio: Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wanaoficha mafuta

Na Tatu Mohamed SERIKALI imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya kuficha...

More like this

NEMC yatoa elimu kwa umma kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Taka Sifuri

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeanza kutoa...

Vijana 521 waondoka kwa ajira nje ya nchi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, hatua...

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....