UWT Njombe wampongeza Rais Samia miaka 47 ya CCM

Na Nora Damian

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Njombe, Scolastica Kevela amepongeza juhudi zinazoonyeshwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuwataka Watanzania kumuunga mkono ili aendelee kuiongoza Tanzania katika kipindi kingine.

Kevela ameyasema hayo leo Februari 5,2024 wakati akizungumzia maadhimisho ya miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema miongoni mwa mambo mengi ya kupongezwa ni katika ujenzi wa demokrasia nchini na kusema Rais Samia amekuwa akitumia busara na hekima katika uongozi wake.

“Amekuwa ‘role model’ katika uongozi kitaifa na kimataifa, sisi wanawake wa Mkoa wa Njombe tunasema 2025 kuelekea 2030 ni Dokta Samia Suluhu Hassan, tunamuunga mkono kwa sababu tunaona anayoyafanya…tuna amani, utulivu, nchi imetulia.

“Kupitia Rais Samia sisi wanawake katupaisha, katupatia makatibu tawala, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wabunge na anaelekea kutupeleka kwenye 50 kwa 50. Tunamuombea aendelee kufanya kazi vizuri na sisi tuko nyuma yake kuhakikisha tunafanya kazi kwa bidii,” amesema Kevela.

Amewataka Watanzania waendelee kukiunga mkono CCM ili kiendelee kushika dola kwa sababu yapo ya kujivunia chini ya utawala wake.

“Miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi inaonyesha namna gani chama kilivyo imara na kitaendelea kushika hatamu kwa sababu lengo letu ni kuisogeza Tanzania mbele.

“Mama kaleta Royal Tour inatuletea watalii wengi, sasa Tanzania inajulikana kitaifa na kimataifa, miaka ya nyuma watu walikuwa wanasema Mlima Kilimanjaro uko Kenya lakini sasa hivi wanatoka huko wanajua uko Tanzania.

“Mikopo ya elimu ya juu hadi wanaosoma diploma wanapata, elimu bure inatolewa hadi kidato cha sita…haya ni maendeleo makubwa,” amesema.

Amesema wanaendelea kushiriki kwa vitendo katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuongeza idadi ya wanachama wapya.

spot_img

Latest articles

GST yaongeza kasi ya tafiti za kijiosayansi kuvutia uwekezaji sekta ya madini

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeongeza kasi ya...

UDSM wabuni mfumo wa simu janja unaosaidia wakulima kutumia maji kwa ufanisi

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimebuni mfumo wa kidijitali unaotumia...

UDSM yahamasisha uwekezaji katika ufugaji wa nyuki wasiodunga

Na Mwandishi Wetu CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimesema Tanzania ina fursa...

DIB yawahakikishia wananchi usalama wa amana zao

Na Mwandishi Wetu BODI ya Bima ya Amana (DIB) imewahakikishia wananchi kuwa fedha wanazoweka...

More like this