DAWASA YATEGUA KITENDAWILI GHARAMA UONDOSHAJI MAJITAKA KIGAMBONI

Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kigamboni wanatarajiwa kupunguza gharama za uondoshaji wa majitaka baada ya DAWASA kukamilisha ujenzi wa mitambo miwili midogo ya kuchakata majitaka katika Kata za Vijibweni na Gezaulole zenye wakazi zaidi ya 410,400.

Mitambo hiyo yenye thamani ya Sh2.3 bilioni imejengwa kwa ajili ya kuchakata majitaka kutoka maeneo hayo, pamoja na kuhudumia magari yanayofanya shughuli za uondoshaji majitaka katika Wilaya ya Kigamboni.

Meneja wa Miradi ya Majitaka DAWASA, Mhandisi Eric Mutalemwa, amesema mitambo hiyo imekamilika, imefanyiwa ukaguzi na sasa iko tayari kuanza kutumika.“Miradi hii ya Vijibweni na Gezaulole ni ya kisasa ya kuchakata majitaka. Tumekagua na kujiridhisha na ukamilishaji wake na sasa iko tayari kutumika kuhudumia wananchi na watumiaji wa magari ya uondoshaji majitaka katika Wilaya hii,” amesema.

Ameongeza kuwa kukamilika kwa mitambo hiyo kutasaidia kupunguza gharama ambazo wakazi wa Kigamboni na watoa huduma binafsi wamekuwa wakitumia kusafirisha majitaka hadi mabwawa yaliyoko mbali na eneo hilo.

Dereva wa gari la uondoshaji majitaka Kigamboni, Habibu Ally, amesema mradi huo utapunguza gharama za uendeshaji kwa kuwa magari hayatakuwa na ulazima wa kusafirisha majitaka hadi Vingunguti na Kurasini.

“Awali ilitulazimu kwenda hadi katika mabwawa ya majitaka Vingunguti na Kurasini. Umbali huo ulifanya tozo kuwa kubwa kwa wateja na kuongeza gharama za uendeshaji wa magari. Mitambo hii itatusaidia kumwaga majitaka hapa hapa Kigamboni na kutupunguzia gharama,” amesema.

Kukamilika kwa mitambo hiyo kunaongeza uwezo wa huduma za usafi wa mazingira Kigamboni na kupunguza umbali wa usafirishaji wa majitaka kwa wananchi na watoa huduma.

spot_img

Latest articles

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA UFANISI

Na Mwandishi Wetu, Tabora TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa...

TANZANIA NA OMAN KUIMARISHA USHIRIKIANO WA WANAHABARI KUPITIA KONGAMANO LA OKTOBA MOSI

DAR ES SALAAM Chama cha Waandishi wa Habari cha Oman (OJA), kwa kushirikiana na Chama...

C-CEOs Forum kuwa chachu ya utekelezaji wa Dira 2050

Na Mwandishi wa OTR Arusha. Serikali imesema Mkutano wa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu...

Media Brains, KAS zawajengea uwezo waandishi kutambua habari feki, washiriki   wafunguka walivyonufaika na mafunzo

Na Winfrida Mtoi Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

More like this