Rais Samia amuasili mtoto mchanga aliyetelekezwa Nzega

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ,Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto mchanga wa kike leo Machi 11, 2026, katika makazi yake, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Mtoto huyo aliyepewa jina la Grace Samia Suluhu Hassan alitelekezwa mjini Nzega, mkoani Tabora, na amekabidhiwa kwa Rais Samia na Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi mtoto huyo, Mkuu wa Wilaya Tukai amesema mtoto huyo aliokotwa Januari 11, 2026 akiwa ametelekezwa katika eneo jirani na nyumba ya wageni ya Kasulu, Nzega Mjini.

Ameeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hizo, alishirikiana na Jeshi la Polisi kumchukua mtoto huyo na kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi na uangalizi, huku juhudi za kumtafuta mama yake zikiendelea bila mafanikio.

Rais Samia amemkaribisha mtoto huyo katika familia yake na kuahidi kumpatia malezi, ulinzi na huduma zote muhimu ili akue katika mazingira salama na yenye upendo.

“Wanaotupa watoto hawajui wanalolifanya. Kuliko kumtupa mtoto ni afadhali ukamkabidhi katika mamlaka za kisheria au kituo cha kulelea watoto. Kila mtoto aliyezaliwa ni hazina, na hatuijui kesho yake,” amesema Rais Samia.

spot_img

Latest articles

Beki Yanga afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Na Mwandishi Wetu NAHODHA msaidizi wa timu ya Yanga na mchezaji wa timu ya Taifa...

Rostam aanika maono yake umiliki mpya ya NMG

Na Mwandishi Wetu MFANYABIASHARA na mwekezaji wa Tanzania, Rostam Azizi, ametangaza uwekezaji mkubwa wa kimkakati...

Tanzania Kunufaika na Mradi wa Umoja wa Ulaya wa Kukabiliana na Hatari za Sumu za Kemikali

Na Mwandishi wetu TANZANIA iko katika hatua za awali za upembuzi wa kushiriki katika mradi...

Rostam Aziz ainunua Nation Media ya Kenya

Na Mwandishi Wetu KAMPUNI ya Taarifa Limited inayomilikiwa na mfanyabiashara Rostam Aziz imeingia makubaliano ya...

More like this