VETA Kuongeza Vyuo Kutoka 80 hadi 152 Kufikia 2027

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imetangaza mpango wa kuongeza idadi ya vyuo vyake kutoka 80 vya sasa hadi 152 ifikapo mwaka 2027, hatua inayotarajiwa kuongeza udahili wa wanafunzi hadi kufikia 250,000 kwa mwaka.

Hatua hiyo inalenga kusogeza huduma za mafunzo ya ufundi stadi karibu zaidi na wananchi na kupanua fursa za ajira kwa vijana nchini.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari uliofanyika leo Februari 16, 2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore, amesema kuwa ujenzi wa vyuo vipya unaendelea katika wilaya 64 pamoja na chuo cha mkoa wa Songwe, huku maandalizi ya ujenzi wa vyuo vitano vya kanda (TVET Polytechnics) yakiwa katika hatua za mwisho.

“Lengo la Serikali ni kuhakikisha kila wilaya inakuwa na angalau chuo kimoja cha VETA ili kuwafikia vijana wengi zaidi, hususan waliopo maeneo ya vijijini,” amesema.

Amefafanua kuwa upanuzi huo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuimarisha elimu ya amali kama nyenzo muhimu ya kuzalisha ajira na kukuza uchumi wa viwanda.

Mbali na kuongeza idadi ya vyuo, CPA Kasore amesema VETA imeendelea kuimarisha miundombinu ya vyuo vilivyopo kwa kujenga karakana, mabweni na madarasa mapya ili kuongeza uwezo wa udahili.

Aidha, amesema taasisi hiyo imeondoa mtihani wa mchujo kwa waombaji wa mafunzo ya muda mrefu, hatua inayolenga kupanua wigo wa upatikanaji wa mafunzo kwa vijana wengi zaidi.

“Katika kuhakikisha mafunzo yanaendana na mahitaji ya soko la ajira, VETA imeendelea kuoanisha mitaala na miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli ya kisasa (SGR), sekta ya madini, gesi na uendelezaji wa bandari. Lengo ni kuwapa wanafunzi uzoefu wa vitendo unaowawezesha kuingia moja kwa moja katika soko la ajira baada ya kuhitimu,” amesema.

CPA Kasore amewahimiza vijana na wazazi kuchangamkia fursa hizo, akisisitiza kuwa ufundi stadi ni mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa na njia ya uhakika ya kujikwamua kiuchumi.Mwisho

spot_img

Latest articles

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...

MD Twange aeleza kutoridhishwa na kasi ya Mkandarasi wa mradi wa Hale

📍Ni ule wa kuboresha kituo cha kufua umeme 📍Amuagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa...

More like this

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Tanesco awahakikishia ushirikiano maafisa huduma kwa wateja

📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye...

Makonda  awajibu wanaoponda ziara ya Rio

Na Winfrida Mtoi WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema ziara ya...

TIRDO yasajili Viwanda 25,650, Yaongeza Maabara za Kisasa Kuimarisha Sekta ya Viwanda

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya...