Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Ukimwi yaipongeza TMDA

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumubya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Dkt. Johanes Lukumay ametoa pongezi kwa uongozi wa TMDA kufuatia kazi nzuri ya udhibiti inayofanywa na Mamlaka ya kulinda afya ya jamii.

Pongezi hizo amezitoa tarehe 12 Februari, 2026 baada ya uwasilishaji wa TMDA wa kazi na majukumu ya taasisi mbele ya Kamati hiyo.

“Kazi ya udhibiti inahitaji umakini mkubwa pamoja na kujitoa kwa dhati ili kusimamia lengo zima la kulinda afya ya jamii,” alisema Dkt. Lukumay.

Naye Mkurugenzi Mkuu, Dkt. Adam Fimbi akiwasilisha mada kuhusu historia, maendeleo na mikakati ya Uimarishaji wa udhibiti wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi, alisema kuwa TMDA inajivunia mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa toka Mamlaka hii imeanzishwa mwaka 2003.

Akiainisha mafanikio yaliyofikiwa Dkt. Fimbo alisema; TMDA imefikia Ngazi ya Tatu ya Umahiri kwrnye mifumo ya Udhibiti wa Dawa (WHO ML3- nchi ya kwanza Afrika 2018), Maabara kutambulika na WHO, Kitivo cha Umajiri cha usajili wa Dawa na udhibiti wa Chanjo Afrika, maabara inatumika kanankitivo cha mafunzo kwa mamlaka nyingine Afrika.

Ametaja mafanikio mengine ni mamlaka kuthibitishwa mifumo yake kwa kiwango cha ISO 9001:2015 na kwa upabde wa Maabara kiwango cha ISO/IEC 17025:2015.

Akichangia mada, Mbunge wa Buchosha Mh. Eric Shigongo anewataka Mamlaka kutoa adhabu kali kwa wanaobainika kuuza au kusambaza dawa duni na bandia.

Naye Mbunge wa Muleba Kaskazini, Adonis Bitegeko, amewataka TMDA kusimamia ipasavyo udhibiti wa dawa za mifugo ili kupunguza usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Akihitimisha tukio hilo la uwasilishaji, Dkt. Lukumay amewataka TMDA kuandaa mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha soko la bidhaa za dawa nchini linakuwa salama na kupunguza utegemezi.

spot_img

Latest articles

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

More like this