Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, (TFF) limeufungia uwanja wa KMC, uliopo Mwenge, jijini Dar es Salaam kutumika kwa mechi za Ligi kutokana na kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Katika taarifa iliyotolewa na Shirikisho hilo leo Januari 29, 2026, imesema miundombinu ya uwanja huo haikidhi matakwa ya Kanuni kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu.
“Kufuatia uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kutumia uwanja mwingine kama Kanuni inavyoelekeza mpaka uwanja wao utakapofunguliwa baada ya kufanyiwa marekebisho na kukaguliwa na TFF,” imesema taarifa hiyo.
Aidha TFF imezikumbusha Klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.
Miongoni mwa timu zinazotumia uwanja huyo kama uwanja wake wa nyumbani katika mechi za Ligi ni Yanga, Tausi Queens na wenyeji KMC.


