Kipa wa zamani Yanga afariki dunia

Na Winfrida Mtoi

KIPA wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Peter Manyika amefariki dunia leo Januari 26, 2025, wakati akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya St. Monica, jijini Dar es Salaam.

Familia kupitia mtoto wake, Manyika JR imethibitisha kuwa baba yake amefariki, mwili umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala, na msiba upo nyumbani kwao Mbezi.

Manyika atakumbukwa katika historia ya soka nchini kama miongoni mwa makipa bora waliojipatia heshima kubwa nchini akiwa na Yanga na timu ya Taifa kuanzia miaka ya mwishoni mwa miaka ya 1980 na 1990.

Mwaka 1999 aliiongoza Yanga kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1999 nchini Uganda.

Baada ya kustaafu soka la ushindani, hakuachana na mchezo huo, aliamua kujikita katika ukocha wa makipa na kuendeleza vipaji, akifanya kazi na klabu  mbalimbali zikiwamo Ihefu, Fountain Gate na timu za taifa za vijana.

Mwaka 2019 klabu yake za zamani, Yanga ilimpa jukumu la kuwanoa makipa wa timu hiyo akichukua nafasi ya Juma Pondamali, kipindi hicho alikuwa ni Metecha Mnata, Faroukh Shikalo, Klaus Kindoki na Ramadhan Kabwili.

spot_img

Latest articles

Twiga, Tanga Cement wapewa saa 48 kujisalimisha

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Wizara ya Madini imezipa Kampuni za Twiga Cement na...

Watendaji wa Uchaguzi watakiwa kutekeleza majukumu kwa weledi

Na. Mwandishi Wetu, Iringa WATENDAJI wa uchaguzi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na weledi...

TCAA yaimarisha usalama wa anga kwa mifumo ya kisasa

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imejizatiti kuendana na mabadiliko...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki kikao cha wadau wa Mahakama

Na Mwandishi Wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari ameshiriki katika kikao cha...

More like this