Mukwala atua Zanzibar, Simba ikiivaa Azam kesho Mapinduzi Cup

Na Winfrida Mtoi

WAKATI Simba kitarajia kukabiliana na Azam FC kesho katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Mapinduzi, mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Uganda Steven Mukwala  amejiunga kikosi hicho  leo na kufanya mazoezi ya mwisho na wenzake.

Mukwala   amerejea kikosini baada ya kumaliza majukumu katika timu ya taifa ya Uganda iliyokuwa ikishiriki fainali za kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2025) ambapo waliishia hatua ya makundi.

Simba imefanya mazoezi ya mwisho katika mazoezi ya mwisho leo Januari 7, 2026 kwenye viwanja vya Maisara, Unguja kujiandaa na mechi hiyo itakayochezwa kesho Alhamisi Januari 8, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, saa 2:15 usiku.

Kuelekea mchezo huo, makocha wa timu hizo mbili zenye upinzani mkali katika Ligi Kuu Tanzania, Steve Barker wa Simba na Florent Ibenge Azam FC wamezungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo mbele ya waandishi wa habari, huku mmoja  akijivunia kikosi chake.

Kocha wa Simba Barker amesema wachezaji wake wana morali ya hali ya juu na wameongezeka kikosini tofauti na walivyoanza, hivyo wamejipanga kucheza vizuri  kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kutinga fainali ikiwezekana kuchukua taji hilo.

Naye kocha mkuu wa Azam FC, Ibenge ameeleza kuwa  anaiheshimu Simba ni kubwa na bora lakini malengo yao katika mechi hiyo ni kuondoka na ushindi.

spot_img

Latest articles

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

More like this