Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuahirisha hafla ya utoaji tuzo za msimu wa 2024/25 ziliyopangwa kufanyika Desemba 5, 2025, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kuahirishwa kumetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa waandaaji ambao ni shirikisho hilo.
“Hatua hii imetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwa sasa. Mara tarehe mpya itakapopangwa mtafahamishwa mara moja”. Taarifa hiyo imeeleza.


