Serikali yaahidi kushirikiana na wadau kuendeleza mchezo wa kuogelea

Na Winfrida Mtoi

WADAU wa mchezo wakuogelea Afrika Mashariki wamekutana kujadili maendeleo ya mchezo huo, huku Serikali ya Tanzania ikiahidi kuunga mkono jitihada zao na kutatua changamoto zilizopo.

Kongamano hilo limefanyika leo Novemba 22, 2025 kwenye ukumbi wa PSSSF Tower jijini Dar es Salaam, likishirikisha zaidi ya watu 100 kutoka Kenya, Uganda na Tanzania.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi inayojihusisha na maendeleo ya michezo ‘ Prime Sports Agency’, wamekutana makocha wa mchezo wa kuogelea, viongozi wa vyama na klabu mbalimbali, wanamichezo na wazazi ambao wamejadili mada mbalimbali.

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara yenye dhamana ya michezo, Boniface Tamba amesema serikali itafanyia kazi yale yaliyojadiliwa na wadau hao ili kuhakikisha mchezo wa kuogelea unapiga hatua nchini.

“Tunashukuru waandaaji wa kongamano hili na watoa mada ambao wametoa mada ambazo zikifanyiwa kazi zitauendeleza huu mchezo wa kuogelea,” amesema.

Tamba amesema serikali inachotakiwa kufanya ni kuwekeza nguvu katika ujenzi wa miundombinu kama vile kujenga bwawa la kuogelea lenye viwango vya Olimpiki.

“Sisi kama serikali mada zote zilizojadiliwa tunazichukua kwa uzito mkubwa, lakini kuna mada moja inayohusu fursa hii inatugusa moja kwa moja, kuna fursa nyingi zinazopatikana katika mchezo wa kuogelea.

Naye Mkurugenzi wa Elimu na Maendeleo wa Chama cha Mchezo wa Kuogelea Tanzania(TSA), Jeremiah Keema amesema matarajio yao baada ya kongamano hilo ni kuona ongezeko la wachezaji hasa katika mashindano ya kimataifa.

“Tuna imani kila mmoja atapata ujuzi zaidi kuhusu mambo yanayohusu mchezo wa kuogelea, baada ya hapa viongozi watapeleka katika vyama vyao, kupitia kamati zao watajenga mkakati wa muda mrefu wa kuandaa wachezaji,” amesema.

Mshiriki kutoka Uganda Max Kanyerezi ameeleza kuwa kukutana kwao ni muhimu katika kujenga uhusiano na kuimarisha ushirikiano wa kukuza mchezo huo kikanda.

“Ndani ya miaka sita Uganda mwamko wa mchezo wa kuogelea umekuwa mkubwa, watoto wanaofanya mazoezi wamefikia 3000 sasa. Kitu kama hiki ndio tunataka kushirikiana na wenzetu wa Afrika Mashariki ili kuwa sawa na kufanya vizuri kimataifa kwa sababu kule wanaangalia ubora kikanda.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Simbo Awinia amesema kuogelea si mchezo tu bali ni muhimu kuwafundisha watoto kwa sababu inawasaidia kiafya, usalama katika mazingira ya maji kama bahari, mito na hata kipindi cha majanga mafuriko ambapo pia wanaweza kuwaokoa wenzao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Prime Sports Agency, Lameck Borega amefurahishwa na muitikio wa washiriki katika kongamano hilo, akisema ni mafanikio kwao kama waandaaji kwa kuwa hata Serikali imeahidi kutoa ushirikiano kufikia malengo wa yale waliyojadili.

“Tunajua mchezo wa kuogelea ni sayansi kwa sababu unafanyika ndani ya maji kwa hiyo ili kufikia malengo lazima makocha wawe na elimu ndio maana tumeleta wataalamu kutoka Afrika Mashariki ambao wana leseni za World Aquatics ambayo ni kama FIFA kwenye mpira,” ameeleza Borega.

spot_img

Latest articles

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...

Mexico yatwaa taji la Miss Universe 2025, Ivory Coast namba tano

Na Mwandishi Wetu Mexico imeibuka mshindi wa taji la Miss Universe 2025 kupitia mrembo wake...

Kocha Yanga ataja mbinu kuingamiza FAR Rabat

Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Concalves amesema falsafa yake katika mechi ya...

Zawadi za PIKU zafungua milango ya ujasiriamali kwa Watanzania

Na Mwandishi Wetu KATIKA kudhihirisha kuwa teknolojia inabadilisha maisha ya Watanzania, Jukwaa la Kidijitali...

More like this

Dube awapa raha wananchi

Na Winfrida Mtoi BAO pekee lililofungwa na Prince Dube dakika ya 58, limeipa Yanga alama...

Mexico yatwaa taji la Miss Universe 2025, Ivory Coast namba tano

Na Mwandishi Wetu Mexico imeibuka mshindi wa taji la Miss Universe 2025 kupitia mrembo wake...

Kocha Yanga ataja mbinu kuingamiza FAR Rabat

Na Mwandishi Wetu KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Concalves amesema falsafa yake katika mechi ya...