Na Mwandishi Wetu
Mexico imeibuka mshindi wa taji la Miss Universe 2025 kupitia mrembo wake Fatima Bosch, mwenye umri wa miaka 24.
Fatima, anafahamika kwa uthubutu wake licha kuishi na hali ya Dyslexia na ADHD, ambapo amegeuza uzoefu wake kuwa nguvu ya kuhamasisha na kutetea watoto, wahamiaji na jamii zilizo katika mazingira hatarishi.
Mrembo huyo ambaye pia ni mbunifu wa mavazi na amekuwa akijitolea katika shughuli mbalimbali kwa muda mrefu.
Katika tano bora, Thailand imeshika nafasi ya pili, first, ikifuatiwa na Venezuela, Philippines ya nne, na Ivory Coast ikishika namba tano.
Katika shindano hilo la 74 la Miss Universe Tanzania lilifanyika usiku wa leo Novemba 21, 2025, katika ukumbi wa Impact Challenger Hall mjini Pak Kret, Nonthaburi, Thailand, Tanzania iliwakilishwa na Naisae Yona.


