Na Winfrida Mtoi
Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Novemba 22,2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex.
Yanga imeondoka leo Novemba 18, 2025 jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani humo, ikiwa na baadhi ya wachezaji kutokana na wengine kuwa katika majukumu ya timu zao za taifa ambao wanatarajiwa kujiunga na timu muda wowote.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Pedro Goncalves amesema wachezaji hao watafika kwa wakati unaotakiwa kujiandaa mchezo huo.


