Jaji Mwambegele afanya ukaguzi wa vifaa vya Uchaguzi Mbeya

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Septemba 19, 2025 ametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika Majimbo ya Uchaguzi ya Mbeya Mjini na Uyole na kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Jaji Mwambegele pia alipata fursa ya kutembelea kampeni za wagombea Ubunge wa chama cha CUF na CCM katika majimbo hayo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Kauli Mbiu ni “Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura”

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this