Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, amemteua mwandishi wa habari, Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), baada ya kamati ya awali kumaliza muda wake.
Nyembera ataiongoza kamati hiyo ya muda ya TPBRC, yenye jumla ya wajumbe sita akiwamo Makamu wake Jacob Mbuya .
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo Agosti 15, 2025 Profesa Kabudi ameipa kamati hiyo siku 90 (kuanzia Julai 29 hadi Oktoba 29) kukamilisha marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi mkuu.
Wengine walioteuliwa ni Gordon Nsajigwa (Katibu), wajumbe ni Shafii Dauda, Irene Mwasanga na Ibrahim Abbas Kamwe.