INEC yatangaza ratiba ya vyama kuchukua fomu za wagombea wa Urais

Na Mwandishi Wetu

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza ratiba ya kuchukua fomu za uteuzi kwa wagombea wa vyama 14 vya siasa waliopendekezwa kugombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zoezi linaloanza kesho Agosti 9, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi wa INEC, Kailima Ramadhani, alisema kuwa kesho fomu zitachukuliwa na wagombea kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), National Reconstruction Alliance (NRA) na Alliance for African Farmers Party (AAFP).

“Hadi leo tarehe 8 Agosti 2025, tumepokea barua kutoka vyama vya siasa 14 zikiainisha tarehe na muda ambao wagombea wao watakuja kuchukua fomu katika ofisi za Tume zilizopo Njedengwa, Dodoma,” amesema Kailima.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, vyama vitakavyofuata ni Chama cha MAKINI (10 Agosti), The National League for Democracy – NLD (10 Agosti), United Peoples’ Democratic Party – UPDP (10 Agosti), na African Democratic Alliance Party – ADA–TADEA (11 Agosti).

Vingine ni Union for Multiparty Democracy – UMD (11 Agosti), Tanzania Labour Party – TLP (11 Agosti), Chama Cha Kijamii – CCK (12 Agosti), Chama cha Ukombozi wa Umma – CHAUMMA (12 Agosti), Alliance for Democratic Change – ADC (12 Agosti), Democratic Party – DP (13 Agosti) na National Convention for Construction and Reform – NCCR–MAGEUZI (15 Agosti).

Kailima amesema Tume imeandikia vyama hivyo barua rasmi kuhusu ratiba ya utoaji fomu na kusisitiza kuwa orodha hiyo inahusu vyama vilivyowasilisha taarifa zao kufikia leo.

Amesema endapo vyama vingine vitajitokeza, ratiba mpya itaandaliwa.Amevitaka vyama kuendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 kwa kuzingatia katiba, sheria na kanuni za uchaguzi, huku akivipongeza kwa maandalizi yanayoendelea.

spot_img

Latest articles

DAWASA yafafanua sababu ya ukosefu wa maji maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)...

Tanesco yatambuliwa kama sekta wezeshi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

📍Yapokea cheti cha pongezi kwa mchango wake katika kuendeleza elimu jumuishi 📍Utambuzi watolewa katika hafla...

DAWASA yaanza kufunga Pampu zitakazoimarisha huduma ya Maji

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA),...

TPDC Yahimiza Wananchi Kulinda Miundombinu ya Bomba la Gesi Asilia

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuwashirikisha wananchi...

More like this