Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amefariki dunia leo Agosti 6,2025 akiwa akiwa anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, imethibitisha Ndugai kufariki ambapo Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson amtoa pole kwa familia na wananchi wa Jimbo la Kongwa.
“Kwa masikitiko makubwa, naomba kutoa taarifa ya kifo cha kiongozi wetu, mwanasia mkongwe na Spika Mstaafu wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai kilichotokea lei jijini Dodoma. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu na jamaa na wananchi wa Jimbo la Kongwa, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu”, amesema Dk Tulia.
Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu November 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.
Ndugai ambaye amezaliwa January 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 5690.