Wanahabari watakiwa kuhamasisha ushiriki wa wananchi Uchaguzi Mkuu 2025

Na Tatu Mohamed

MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele, amewataka waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, huku wakilinda amani, mshikamano na maadili ya kitaifa.

Hayo ameyasema leo Agosti 2, 2025 kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, kati ya waandishi wa habari na Tume hiyo.

Jaji Mwambegele amesema waandishi wa habari ni daraja muhimu kati ya Tume na wananchi, hivyo wanayo nafasi ya kipekee ya kusaidia katika kutoa elimu ya mpiga kura, kufikisha taarifa sahihi, na kuchangia mchakato wa uchaguzi kwa weledi.

“Tume inawatambua ninyi waandishi wa habari kama daraja la mawasiliano kati ya Tume na umma, lakini pia kama wadau muhimu wa uchaguzi. Mnachangia kwa kiasi kikubwa kuripoti habari za maandalizi, kampeni, upigaji kura na matokeo,” amesema Jaji Mwambegele.

Amewahimiza waandishi wa habari kuendeleza ushirikiano na Tume, kwa lengo la kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025 unafanyika kwa uhuru, haki, uwazi na kuaminika.

“Kauli mbiu yetu ni: ‘Kura Yako Haki Yako – Piga Kura.’ Tume ina matumaini makubwa ya kufanikisha uchaguzi huu kwa kushirikiana nanyi katika kila hatua,” amesema.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, NEC imeshatangaza ratiba rasmi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ambapo utoaji wa fomu kwa wagombea wa ubunge na udiwani utaanza Agosti 9 hadi Agosti 27, huku wagombea wa urais na makamu wao wakitarajiwa kuchukua fomu kati ya Agosti 14 hadi 24.

“Uteuzi wa wagombea wote utafanyika Agosti 27.Kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 28 hadi Oktoba 27 kwa upande wa Tanzania Bara, na hadi Oktoba 28 kwa upande wa Zanzibar,” amesema.

Jaji Mwambegele amewaasa wanahabari kutumia vyombo vyao kuhamasisha kampeni za kistaarabu zinazojenga hoja na siyo chuki au uchochezi.

“Katika kipindi hiki cha kampeni, mnapaswa kuhakikisha kuwa vyombo vyenu havitumiwi kuvuruga amani ya nchi. Toeni taarifa za haki, za kweli, na zenye kujenga jamii,” amesisitiza.

Ameeleza kuwa mwaka 2024, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria mbili muhimu: Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, pamoja na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.

“Kupitia sheria hizo, Tume imetunga kanuni na miongozo ya kuendesha uchaguzi wa mwaka huu. Aidha, Tume imetoa mwongozo wa elimu ya mpiga kura, mwongozo kwa vyombo vya habari, na nakala za sheria husika kwa wadau wote, ili kuwawezesha kufuata taratibu ipasavyo.

“Nawasihi msome na kuelewa nyaraka hizi ili mchango wenu katika uchaguzi huu uwe wa manufaa kwa taifa,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa, kwa lengo la kuongeza weledi katika kuripoti shughuli za uchaguzi, Tume imeandaa mafunzo maalum kwa wahariri na waandishi wa habari yatakayofanyika Agosti 4, 2025.

Naye Mwandishi wa habari kutoka ITV, Godfrey Monyo alishukuru INEC kwa mafunzo hayo ambayo yataweza kuwasaidia.

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwetu hasa katika kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu… kwahiyo sisi kama waandishi wa habari tutahakikisha tunafanya kazi zetu kwa weledi pamoja na kuzingatia Sheria zilizowekwa,” amesema.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

Hizi ndizo hisia dhidi ya INEC, Msajili wa Vyama vya Siasa

KATIKA safu hii wiki iliyopita niliandika uchambuzi nikihoji, ‘INEC, Msajili wa Vyama wanaweza kutupa...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...