Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Simba leo Julai 30, 2025, imemtambulisha Alassane Kante raia wa Senegal , akitokea CA Bizertin ya Tunisia.
Kiungo huyo mkabaji mwenye umri wa miaka 24, amesaini mkataba wa miaka miwili.
Wanamsimbazi hao walianza rasmi jana kuanika usajili wao kwa kumtambulisha beki Rushine De Reuck raia wa Afrika Kusini akitokea klabu ya Mamelody Sundowns.