Mbaroni kwa kumuua mama mkwe na kumjeruhi mkewe

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia Jumanne Kibagi, mkazi wa kijiji cha Nyarufu wilayani Bunda kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake  iatwaye  Kabula Masanja (50) na kumjeruhi mkewe  Nyangeta Kunyaranyara (21) kwa kutumia panga.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, tukio hilo limetokea Julai 19, 2025  majira ya saa  7;30 usiku katika kijiji cha Chumwi kilichopo wilayani Musoma, ambapo chanzo kimetajwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia kati ya mtuhumiwa na mke wake.

Inadaiwa kuwa  Nyangeta ambaye ni mke wa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu mume wake kujihusisha na  vitendo vya kihalifu hususani wizi hali iliyosababisha mwanamke huyo kukimbilia nyumbani kwa mama yake ambapo mtuhumiwa aliwafuata huko  na kuwashambulia kwa kuwakata mapanga sehemu mbalimbali.

“Majirani walifanya jitihada za kuwapeleka katika kituo cha afya Murangi kwa  jailli ya kupatiwa matibabu ambapo Kabula Masanja alifariki akiwa anaendelea na matibabu,” imesema taarifa hiyo.

Akizungumzia tukio hilo, mke wa mtuhumiwa, Nyangeta, akiwa katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ameeleza kuwa mtuhumiwa alifika nyumbani kwao usiku na kutekeleza tukio hilo.

Amesema Jumanne alikuwa mume wake ambaye waliishi pamoja kwa muda wa mwaka mmoja, na waliachana baada ya kugundua mwanaume huyo anajihusisha na matukio ya kihalifu.

Nyangeta amesema kabla ya tukio hilo, Jumanne alimpigia simu mama yake akimjulisha nia ya kwenda kumchukua mke wake (Nyangeta), ambapo mama yake alikataa, na ndipo siku ya tukio alipovamia na kuwakata panga yeye na mama yake.

spot_img

Latest articles

MADIWANI WA MPANDA NA NSIMBO WAIPONGEZA SERIKALI KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA JULIUS NYERERE

Na Mwandishi wetu Rufiji - Pwani MADIWANI wa Halmashauri za Wilaya za Mpanda na Nsimbo mkoani...

WANANCHI MSIHOFU KUTUMIA NISHATI YA UMEME KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI -MD TWANGE

📌Asema TANESCO inajenga vituo vya kuchajia vyombo hivyo nchi nzima 📌Aeleza mpango wa kusambaza majiko...

Aibu: Ukaburu waibuka Baraza la Wawakilishi

MSIMU wa siasa za masimango na kubaguana umerejea tena na kushika kasi. Safari hii...

More like this