Na Mwandishi Wetu
Mabingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania, Klabu ya Yanga imemtambulisha rasmi kiungo wa kimataifa wa Guinea, Moussa Bala Conte kutoka klabu ya CS Saxfien ya Tunisia, amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Kiungo huyo aliyetambulishwa rasmi leo Julai 18,2025 na Wanajangwani hao, alikuwa akihusishwa pia kujiunga na Simba.

Conte amekuwa na msimu mzuri akiwa na timu yake ya CS Sfaxien, akitanjwa kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mshambuliaji au mchezeshaji.