Rais Mwinyi afungua Jengo Jipya la Tume ya Uchaguzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi Jengo jipya na la kisasa la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) lililopo Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kuimarisha mazingira bora ya utendaji wa taasisi hiyo muhimu kwa demokrasia nchini. 

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 16 Julai 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo hilo, ambapo pia alifungua Afisi ya Wilaya ya Magharibi “B”, na kusisitiza kuwa ujenzi wa majengo hayo ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2020. 

Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haikusita kugharamia ujenzi wa makao makuu ya Tume hiyo pamoja na afisi za wilaya, kwa kutambua umuhimu wa taasisi hiyo katika kuhakikisha chaguzi huru, haki na wa kuaminika. 

Kwa mujibu wa taarifa ya kitaalamu, Dkt. Mwinyi amesema kuwa Serikali imetoa jumla ya Bilioni 14,1 kwa ajili ya mradi huo uliojengwa na kampuni ya ujenzi ya CRJE na kutoa wito kwa watendaji wa Tume hiyo kuzitunza ofisi hizo ili ziendelee kuwa katika ubora wa hali ya juu. 

Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza Tume hiyo kwa kuendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa ustadi mkubwa, ambapo uandikishaji wa wapiga kura ulifanyika kwa utulivu.

Amehimiza wananchi ambao hawajachukua vitambulisho vyao vya kupigia kura kutimiza wajibu wao  na  kuhakikisha wanatumia haki yao ya kidemokrasia kwa utulivu na kuilinda amani ya nchi. 

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar umemtunukia Rais Dkt. Mwinyi tuzo maalum ya kutambua utendaji na juhudi zake za kuimarisha demokrasia nchini pamoja na kukamilika kwa jengo hilo. 

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wakuu wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Watendaji  wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Viongozi wa vyama vya Siasa, Taasisi za Ujenzi, pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba.

spot_img

Latest articles

Kamati ya kudumu ya Binge Nishati na Madini yaridhishwa na maendeleo ya Kiwanda cha nguzo za zege

📌Ni mradi wa kihistoria kutekelezwa chini ya Serikali ya awamu ya Sita 📌 Yaipongeza...

Waziri Ulega, RC Chalamila pekueni mafaili wizarani

KWA nyakati tofauti viongozi wawili wamezungumzia jiji la Dar es Salaam kuhusu msongamano wa...

Rais Samia amuasili mtoto mchanga aliyetelekezwa Nzega

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ,Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto...

Beki Yanga afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Na Mwandishi Wetu NAHODHA msaidizi wa timu ya Yanga na mchezaji wa timu ya Taifa...

More like this