PURA yajivunia mafanikio katika Ajenda ya Nishati Safi na ushiriki wa Watanzania Sekta ya Mafuta na Gesi

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Kudhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imesema inajivunia utekelezaji wa agenda ya Nishati Safi ya kupikia iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa imeanza kutekelezwa kwa vitendo na kuonyesha mafanikio makubwa.

Akizungumza katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Charles Sangweni, amesema mwitikio wa wananchi kuhusu nishati safi umekuwa mkubwa, na kwamba mamlaka hiyo imejipanga kuhakikisha haina mwanya wa kumuangusha Rais katika agenda hiyo muhimu ya kitaifa.

“Katika maonesho haya ya Sabasaba, tumeona mwamko mkubwa wa wananchi katika masuala ya nishati safi ya kupikia. Hii inaonyesha uelewa unaongezeka, na sisi kama PURA tunaitekeleza agenda hii kikamilifu,” amesema Sangweni.

Ameeleza kuwa PURA imekuwa mshiriki wa kudumu wa maonesho hayo tangu mwaka 2017, na kwamba kila mwaka kumekuwa na maboresho ya kimkakati katika ushiriki wao.

Kwa mwaka huu, amesema, mambo yameimarika zaidi, hasa kwenye matumizi ya mifumo ya kidijitali na ongezeko la idadi ya wananchi wanaotembelea banda lao.

“Watu wanauliza maswali ya msingi, yenye maana na yanayoonyesha namna uelewa kuhusu sekta ya mafuta na gesi ulivyopanuka. Tunapokea maoni, changamoto na maulizo ambayo yanatusaidia pia kuboresha utendaji wetu,” amesema.

Akizungumzia nafasi ya Watanzania katika sekta ya mafuta na gesi, Sangweni amesema tangu kuanzishwa kwa PURA, kumekuwa na ongezeko kubwa la ushiriki wa Watanzania, ambapo kwa sasa asilimia 85 ya ajira katika sekta hiyo zinashikiliwa na wazawa, ikilinganishwa na chini ya asilimia 55 hapo awali.

“Uzoefu na uelewa vimeongezeka. Awali meli zilikuja na wafanyakazi kutoka nje pekee, lakini sasa hata Watanzania wapo ndani ya timu hizo. Hili ni jambo la kujivunia,” amesema.

Kwa mujibu wa Sangweni, PURA kwa sasa iko kwenye maandalizi ya kuchimba visima vitatu katika eneo la Mtwara, huku ushiriki wa Watanzania katika vitalu hivyo ukiwa umefikia asilimia 40.

Pia amesema kati ya kampuni 10 zinazofanya utafiti wa mafuta na gesi nchini, sita zinamilikiwa na Watanzania.

“Kwenye nafasi za uongozi ndani ya sekta, karibu asilimia 95 zinashikiliwa na Watanzania. Hii inadhihirisha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha rasilimali zetu zinawanufaisha wananchi,” amesema.

Ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji na ushirikishwaji wa Watanzania katika miradi ya kimkakati, akisisitiza kuwa PURA itaendelea kuhakikisha kila hatua ya maendeleo inawagusa Watanzania moja kwa moja.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...