PSPTB yatangaza Mitihani ya 31 ya Kitaaluma, Usajili kufungwa Agosti 15, mwaka huu

Na Tatu Mohamed

BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetangaza kuendesha Mitihani ya 31 ya kitaaluma kuanzia tarehe 25 hadi 29 Agosti, 2025, jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha taaluma na uwajibikaji katika sekta ya ununuzi na ugavi nchini.

Akizungumza Julai 4, 2025, wakati wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB, Godfred Mbanyi, alieleza kuwa usajili wa mitihani hiyo tayari umefunguliwa rasmi kupitia tovuti ya bodi hiyo (https://registration.psptb.go.tz) na utahitimishwa tarehe 15 Agosti, 2025.

“Tunawaalika waombaji wote wenye sifa kujiandikisha mapema na kujiandaa kupitia madarasa ya maandalizi. Mitihani hii ni muhimu kwa kukuza taaluma na kuongeza ufanisi katika utendaji wa sekta ya ununuzi,” alisema Mbanyi.

Amefafanua kuwa waombaji wanaostahili ni pamoja na wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi kwa ngazi zote (Astashahada, Stashahada, Shahada), wafanyakazi wa umma na binafsi wanaotekeleza majukumu ya ununuzi bila vyeti rasmi vya kitaaluma, pamoja na waliowahi kufanya mitihani ya PSPTB awali na wanarudia au wanaendelea na ngazi zinazofuata.

Mbanyi alieleza kuwa watahiniwa wanaorudia mitihani zaidi ya ngazi moja wanaruhusiwa kuunganisha ngazi mbili zinazofuatana (Two Consecutive Blocs), kwa idadi ya masomo kati ya mawili hadi sita, kulingana na ratiba rasmi ya Mitihani ya 31.

Kuhusu ada, PSPTB imetoa maelezo kwenye tovuti yao rasmi, huku ikihimiza waombaji kutembelea ukurasa huo kwa taarifa zaidi.

Mbanyi alisisitiza kuwa mitihani mingine ya kawaida inayofanyika mwezi Mei na Novemba itaendelea kama kawaida kwa mujibu wa ratiba ya bodi hiyo.

“Lengo letu ni kuhakikisha sekta ya ununuzi na ugavi inakuwa na wataalam wenye viwango, wanaotambulika kisheria na kitaaluma. Hili ni eneo nyeti katika matumizi ya rasilimali za umma na tija ya taifa kwa ujumla,” alisema.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...