Dkt. Kazungu: Nishati Safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia, Wizara inaitekeleza kwa vitendo

📌Apokea Magari Mawili kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanza kampeni ya kutoa elimu ya uhamasishaji wa nishati safi ya kupikia nchi nzima

📌 Amshukuru Dkt Samia kwa kuwa kinara wa nishati safi na kuibeba ajenda hiyo

📌 Umoja wa Ulaya waridhishwa na jitihada za Tanzania kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia

📌UNCDF yaahidi kushirikiana na Wizara kuhakikisha watanzania wanafikiwa na elimu ya nishati safi

Na Mwandishi Wetu

NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati Jadidifu, Dkt Khatibu Kazungu leo 04 Julai, 2025 amepokea magari mawili yatakayotumika kwa ajili ya kampeni ya kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia chini ya kampeni ya nishati safi ya kupikia Okoa Maisha na Mazingira itakayoendeshwa nchi nzima na Wizara ya nishati kwa kushirikiana na UNCDF.

‘’ Ajenda ya Nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia na sisi Wizara ya Nishati tuko tayari kwa utekelezaji ili kumuunga mkono Mhe. Rais Samia’’ amesema Dkt. Kazungu.

Aidha, ameishukuru Umoja wa Ulaya, na UNCDF kwa kutekeleza mradi wa nishati safi ya kupikia chini ya mfuko wa Cook fund kwa kuwa umesaidia kubadili maisha na mitazamo ya wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya Nishati safi.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Balozi wa Umoja wa Ulaya, Balozi Christine Grau amesema umoja wa Ulaya uko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania kwenye utekelezaji wa Nishati safi ya kupikia na tayari EU imetoa kiasi cha Euro Milioni 19.4 sawa na shilingi Bilioni 59 kutekeleza miradi ya nishati safi ya kupikia kwa mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Pwani, Morogoro na Mwanza.

Kuhusu magari amesema magari hayo mawili yana thamani ya Euro 130,000 na amewataka wizara ya Nishati kuhakikisha wananchi wa vijijini wanafikiwa na nishati safi ya kupikia.

Tanzania inajipanga kutekeleza kwa vitendo mkakati wa Taifa wa Nishati safi ya kupikia chini ya mkakati wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa elimu kwa wananchi na kufikia lengo la Serikali la asilimia 80 ya watanzania kuanza kutumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

spot_img

Latest articles

FILAMU YA ‘THE RHINO OF NGORONGORO’ YAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro KATIKA kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, inayoadhimishwa Septemba 22 kila mwaka,...

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...

ASKARI NA MAHABUSU WADAIWA KUFARIKI AJALI YA GARI LA POLISI MLIMA SEKENKE

Na Mwandishi Wetu ASKARI na mahabusu wanadaiwa kufariki dunia baada ya gari la Polisi walilokuwa...

More like this

FILAMU YA ‘THE RHINO OF NGORONGORO’ YAZINDULIWA

Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro KATIKA kuadhimisha Siku ya Faru Duniani, inayoadhimishwa Septemba 22 kila mwaka,...

Rais Samia atuma salamu za rambirambi vifo vya polisi na mahabusu

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma...

NSSF YAWEKA MKAKATI WA KUFIKISHA WANACHAMA MILIONI 6.6

Na Tatu Mohamed MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeweka mkakati wa kuongeza...