Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaweka wazi nafasi yake kwenye Uchaguzi Mkuu

Na Tatu Mohamed

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imesema kuwa ina wajibu kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unakuwa huru na wa haki nchini.

Hayo yameelezwa na Kamishna Mkazi wa Tume Zanzibar, Khatib Mwinyichande, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere.

Alisema Sabasaba ni fursa muhimu ya kuwa karibu na wananchi, kupokea malalamiko yao, na kuwaelimisha kuhusu haki zao za msingi.

“Maonyesho haya yanatupa nafasi ya kukutana moja kwa moja na wananchi. Tunalinda haki zao, tunawaelimisha kuhusu wajibu wao, na tunawakumbusha kuwa hakuna mtu anayepaswa kunyimwa haki yake kwa misingi yoyote,” alisema Kamishna Mwinyichande.

Aidha, alieleza kuwa Tume hiyo, kama chombo huru cha kikatiba, ina wajibu wa kuhakikisha uchaguzi mkuu nchini unakuwa huru, wa haki na unaozingatia misingi ya utawala bora.

“Uchaguzi si tukio la kisiasa tu, bali ni haki ya msingi kwa wananchi. Tume yetu ina jukumu la kuhakikisha kuwa mchakato wote wa uchaguzi unazingatia sheria, haki za binadamu na misingi ya demokrasia,” alibainisha.

Mwinyichande alisema Tume itakuwa miongoni mwa waangalizi wa uchaguzi mkuu, kuanzia kampeni hadi upigaji kura, na itakuwa ikifuatilia mwenendo wa uchaguzi ili kubaini changamoto na mapungufu yanayoweza kuathiri haki za wananchi, kisha kuwasilisha ripoti kwa mamlaka husika kwa ajili ya maboresho ya baadaye.

Alisisitiza kuwa kazi ya Tume si tu kulinda haki baada ya matatizo kutokea, bali pia ni kuzuia ukiukwaji wa haki kabla haujatokea kwa njia ya elimu na ushawishi wa sera zenye mwelekeo wa haki na usawa.

Kwa ujumla, ushiriki wa Tume ya Haki za Binadamu katika Sabasaba mwaka huu umeonesha namna taasisi za umma zinavyoweza kutumia majukwaa ya kijamii kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu haki zao, wajibu wao, na njia salama za kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi kupitia uchaguzi wa kidemokrasia.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...