TMDA yaendelea kuelimisha umma juu ya matumizi sahihi ya dawa Sabasaba

Na Tatu Mohamed

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Imeendelea kutoa Elimu kwa Umma juu ya matumizi sahihi ya Dawa na vitenganishi ndani ya maonesho ya 49 ya Kimataifa ya biashara (SabaSaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Temeke, Dar Es Salaam.

Akizungumza katika banda la Stone town ndani ya maonesho hayo ya Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amesema kama Mamlaka mara kwa mara wataendelea kutoa elimu kwa Umma ili kusaidia Jamii kuwa na uelewa wa matumizi sahihi ya Dawa.

Amesema majukumu makubwa ya TMDA ni kusajili dawa za ndani na zinazotoka nje kuingia nchini hii ni pamoja na kufanya ukaguzi kila siku ikiwemo kwenye maduka ya Dawa, masoko na mipaka ili kumlinda mtanzania.

“Sisi jukumu letu kuhakikisha kwamba dawa inatumika kama ilivyokusudiwa na sio kumdhuru mtumiaji.Majukumu yetu ni kuhakikisha tunasajili dawa zilizosajiliwa na kukidhi soko la nchi yote hii ni kumlinda Mtanzania katika usalama wa dawa hivyo tunahakika ubora na ufanisi.

“Vile vile tunafanya kazi tunapima bidhaa za dawa kupitia Maabara zetu za kisasa ambazo zina ubora wa Kimataifa wa WHO,” amesema Dkt. Adam Fimbo.

Aidha, katika banda hilo la TMDA, Dkt Adam Fimbo ametoa elimu kwa Wananchi waliotembelea juu ya matumizi sahihi ya Dawa na kuacha kutumia bidhaa hiyo kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu ili kuepuka usugu wa dawa.

spot_img

Latest articles

Ridhiwani aipa tano Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na...

Dkt. Kazungu: Nishati Safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia, Wizara inaitekeleza kwa vitendo

📌Apokea Magari Mawili kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kuanza kampeni ya kutoa...

Dk.Jingu awashauri vijana kujiandaa kwa uzee

Na Mwandishi Wetu ‎Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi...

Wagombea  urais watano TFF wapigwa chini abaki  Karia 

Na Mwandishi Wetu Kamati ya Uchaguzi ya TFF imewang'oa wagombea watano wa nafasi ya Urais...

More like this