Majaliwa  atangaza hagombei tena ubunge Ruangwa

Na Mwandishi Wetu

Waziri mkuu na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa leo Julai 2, 2025 ametangaza rasmi kutokugombea tena ubunge wa jimbo la Ruangwa baada ya kulitumikia jimbo hilo kwa miaka 15.

Akizungumza na wajumbe wa kamati ya Siasa ya Mkoa na Wilaya ya Ruangwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa kumuunga mkono wakati wote ambao amekuwa mbunge wa jimbo hilo.

“Imefika wakati kwa mshikamano tulioujenga  sasa ni wakati wa kutoa fursa kwa Wana-Ruangwa wengine wapenda maendeleo waweze kuunganisha nguvu hizi ili Kauli mbiu yetu ya Ruangwa kwa maendeleo inawezekana iweze kusonga mbele zaidi.”

Aidha, ametoa wito wajumbe wa kamati ya siasa ya Wilaya kuwapa ushirikiano wagombea wote wenye nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewasihi Wana-Ruangwa kuendelea kushikamana na itakapofika siku ya uchaguzi waweze kuchagua wagombea wote watakaowakilisha chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo. 

“Viongozi wetu Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Mwenza Dk. Nchimbi watakapokuja tujitokeze kwa wingi kwenye mikutano tusikilize sera, lakini siku ya kupiga kura tuwapigie kura nyingi za kutosha.”

Aidha, amemshukuru RaisSamia  Viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumuamini na kumpa fursa ya kuwatumikia wana Ruangwa.

Majaliwa alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa mwaka 2010 na amehudumu kwa kipindi cha miaka 15.

spot_img

Latest articles

Waziri Ulega, RC Chalamila pekueni mafaili wizarani

KWA nyakati tofauti viongozi wawili wamezungumzia jiji la Dar es Salaam kuhusu msongamano wa...

Rais Samia amuasili mtoto mchanga aliyetelekezwa Nzega

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ,Samia Suluhu Hassan, amemuasili mtoto...

Beki Yanga afanyiwa upasuaji Afrika Kusini

Na Mwandishi Wetu NAHODHA msaidizi wa timu ya Yanga na mchezaji wa timu ya Taifa...

Rostam aanika maono yake umiliki mpya ya NMG

Na Mwandishi Wetu MFANYABIASHARA na mwekezaji wa Tanzania, Rostam Azizi, ametangaza uwekezaji mkubwa wa kimkakati...

More like this