Kihongosi aahidi kutekeleza alichoagizwa na Rais Samia  Arusha

Na Mwandishi Wetu

 Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha,  Kenani Kihongosi amesema  atafanya kazi aliyotumwa na Rais Samia Suluhu Hassani na  hataruhusu kikwazo chochote kitakachojaribu kuzuia maendeleo ya wananchi.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa ofisi leo Juni  30,2025 na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, Kihongosi amesema  ataendeleza pale pale  alipoishia mtangulizi wake ili  kusonga mbele lengo  kila mwananchi wa Arusha aweze kufurahia matunda.

“Mheshimiwa Rais aliponiteua naamini wote mlisikia, kuna kazi alinituma na alizungumza hadharani. Ajenda yetu  kubwa ni  wananchi kuwa na imani na Serikali yao, fedha zinaletwa, miradi inajengwa kazi yetu ni kwenda kuisimamia,” ameeleza.

Aidha Kihingosi  amewaomba watumishi wenzake wa umma kushirikiana katika kazi waliyoaminiwa ili kuhakikisha wananchi wanapa kile walichokitarajia.

“Mhe Rais amenituma Arusha kuja kuwatumikia wananchi wa Arusha na nimekuja kufanya kazi, ninachoomba kwenu ni ushirikiano ili kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo, tukiwa na lengo la kuhakikisha wananchi wa Arusha wanafurahia matunda ya nchi yao,” amesema Kihongosi.

Kwa upande wake, Makonda  wakati akitoa hotuba yake ya kuwaaga wakazi wa Arusha, ameweka wazi kuwa  anavyofahamu uchapakazi wa Kihongosi  na hana mashaka naye na kumtaka kuendelea kuwatumikia wananchi wa Arusha,  huku akimsisitiza umuhimu wa ushirikiano na mshikamano kati yake na viongozi wa mkoa huo wakiwememo viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa dini, wadau na wananchi wa ngazi zote.

“Nina imani kuwa Mkuu mpya wa Mkoa, Mheshimiwa Kenan Kihongosi, ataendeleza jitihada zote tulizoanza na kuongeza ubunifu mpya katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Arusha, nikuhakikishie wananchi wa Arusha wote ni wajanja na wapenda maendeleo” amesema Makonda.

Kihongosi amehamishiwa mkoani Arusha akitokea Mkoa wa Simiyu ambapo  wakati wa kuapishwa  Rais Samia  alimtaka  kutumia nguvu aliyotumia  Simiyu, akatumie Arusha agizo  mojawapo ikiwa ni kuwaunganisha wananchi wa mkoa huo.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...