Simba yawaita mashabiki kwa Mkapa Juni 15

Na Mwandishi Wetu

Pamoja na mkanganyiko uliopo juu ya mchezo dabi ambapo Yanga wameweka wazi kuwa hawatapeleka timu uwanjani Juni 15, klabu ya Simba imetoa taarifa ya kuwaita mashabiki wao kwenda kujaza uwanja siku hiyo wakisisitiza kuwa mechi hiyo itachezwa.

Kwa  mujibu wa taarifa hiyo, iliyotolewa leo Juni 10,2025  mchezo namba 184 wa Ligi Kuu  dhidi ya Yanga uliopangwa kufanyika Juni 15, 2025 upo kama ulivyopangwa.

Uongozi wa klabu hiyo  umewataka wale ambao walinunua tiketi za mechi ya Machi 8, 2025 wazitunze kwa ajili ya matumizi ya mchezo huo na wale ambao hawajanunua tiketi wajiandae kununua baada ya tangazo la Bodi ya Ligi.

“Twendeni tukaujaze Uwanja wa Mkapa. Inafahamika wazi kuwa Ligi Kuu ya NBC inajumuisha Timu 16 na si ligi ya timu moja, kwa mujibu wa taratibu kabla ya kuanza msimu vilabu vyote16 hushiriki vikao na kutoa mapendekezo ya kuboresha kanuni na taratibu ili kuimarisha ligi yetu, hivyo wenye hoja wafuate taratibu husika,” imesema taarifa hiyo ya Simba na kuongeza kuwa

“Tunaomba Bodi ya Ligi na TFF watoe hadharani ripoti ya uchunguzi juu ya wale wote waliohusika kuharibu mechi ya ligi jioni ya tarehe 7/3/2025 na wachukuliwe hatua stahiki na mamlaka husika.

‘Kutotolewa kwa ripoti na kutochukuliwa hatua kwa wanaoendelea kuchochea ghasia ni sawa na kulinda uharamia katika mpira ambao unatia dosari mafanikio yaliyopo katika tasnia ya mpira wa miguu nchini kwa sasa.”

spot_img

Latest articles

Matendo ya Polisi ni hujuma dhidi ya utawala bora, demokrasia

MFUMO wa uchumi wa soko huru una kanuni zake. Miongoni mwake ni kuruhusu ushindani....

Dkt. Mataragio: Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wanaoficha mafuta

Na Tatu Mohamed SERIKALI imetoa onyo kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na vitendo vya kuficha...

Lukuvi afariki dunia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye...

Mgodi wa kihistoria wa niobium kujengwa Mbeya

Na Mwandishi Mbeya TANZANIA imepiga hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Marekani baada...

More like this