Serikali yasisitiza Dabi iko pale pale Juni 15

Na Mwandishi Wetu

Wakati Yanga ikiendelea na kampeni yake ya ‘Hatuchezi’ Serikali imethibitisha rasmi kuwa pambano watani  hao wa jadi,Yanga na Simba litapigwa kama ilivyopangwa, Juni 15, 2025, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika kipindi cha Maswali na Majibu mapema leo Mei 30, 2025, bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, alijibu swali kutoka kwa Naibu Spika, Mussa Hassan Zungu, kuhusu mechi hiyo kutokana na ukarabati mkubwa wa uwanja huo.

Zungu alitaka kufahamu iwapo uwanja wa Mkapa utakuwa tayari kwa mechi hiyo,?

Itakumbukwa kuwa awali, pambano hilo la watani lilikuwa lipigwe Machi 8, Mwaka huu kabla ya kuahirishwa na Bodi ya Ligi (TPLB) na baadaye kupagwa kuchezwa Juni 15, mwaka huu.

Pia  MwanaFA, amesema Tanzania inaendelea na maandalizi ya michuano ya CHAN inayotarajiwa kufanyika nchini hivi karibuni na kuwahakikishia Watanzania na wapenda soka kuwa Tanzania ipo tayari kwa michuano hiyo baada ya kukamilisha ukarabati ya viwanja na maeneo yote muhimu kwa ajili ya michuano hiyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga, aliyetaka kufahamu maandalizi ya michuano hiyo yamefikia hatua gani, Naibu Waziri Mwinjuma amesema ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam upo katika hatua za mwisho pamoja na Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na maeneo ya viwanja vya mazoezi kwa timu zitakazohitaji.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...