Tanzania, Morocco kuongeza ushirikiano sekta ya nishati

📌 Matumizi ya teknolojia kupewa kipaumbele Sekta ya Nishati

📌 Morocco wampongeza Rais Samia kwa usimamizi bora Sekta ya Nishati

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Morocco wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa matumizi ya teknolojia katika Sekta ya Nishati ili kuiwezesha sekta hiyo kuwa na mchango endelevu nchini.

Hayo yamebainishwa leo Mei 14, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati alipokutana na mwenyeji wake Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Leila Benali kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya nishati ili kuimarisha ushirikiano na nchi ya Morocco.

“Mwaka 2016 Tanzania na Morocco zilisaini hati ya makubaliano (MoU) ya kuimarisha ushirikiano katika sekta ya umeme, mafuta na matumizi ya nishati mbadala ili yapewe kipaumbele katika nchi hizo,” amesema Dkt. Biteko.

Amesema pamoja na maendeleo ya nishati yaliyofikiwa, bado nchi inahitaji uwekezaji zaidi katika sekta ya nishati mbadala ikiwa na matarajio ya kukuza shughuli za kiuchumi hususan katika sekta za viwanda na madini jambo ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati zaidi katika sekta ya nishati.

Ameyataja mambo mengine kuwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu miongoni mwa wataalam katika sekta ya nishati ikilenga kuifanya kuwa na tija kwa taifa na uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Waziri wa Mageuzi ya Nishati na Maendeleo Endelevu wa Ufalme wa Morocco, Leila Benali amesema kuwa Tanzania inaweza kubadilisha sura yake kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi.

Amesema hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana gizani hivyo, njia ya kuleta maendeleo na ustawi wa watu ni kuwaangaza maisha yao kupitia sekta ya nishati.Aidha, Benali amepongeza kwa dhati juhudi za Rais Samia kuwa kinara wa maendeleo ya nishati safi ya kupikia, Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko ameongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Ally Mwadini, wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC).

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...