Upanuzi wa Kituo cha Kupoza umeme Mbagala mbioni kukamilika

📌Awamu ya kwanza ya upanuzi wa Kituo Megawati 45 yakamilika

📌Asema wananchi wa Mbagala na Temeke watapata umeme wa uhakika

📌Awataka wananchi wa Mbagala kuendelea kuwa wavumilivu wakati wa utekelezaji wa Mradi

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange amesema wananchi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake sasa wanatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala kuongezewa uwezo kutoka Megawati 45 za awali na kufikia Megawati 165.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Kituo hicho, Twange alisema kuwa Kituo hicho kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali hivyo kitakuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza umeme na kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

“Kituo hiki kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali na mpaka sasa utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 70. Wananchi wa Mbagala na viunga vyake sasa wategemee umeme wa uhakika’’ amesisitiza Twange.

Pia, Mkurugenzi Mtendaji, Lazaro amemshukuru sana Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani milioni 6.4 ili kufanikisha Mradi huu wenye tija na manufaa kwa wananchi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda, akizungumza wakati wa ziara hiyo amepongeza jitihada zinazofanywa na TANESCO ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kumaliza kero ya umeme katika maeneo mengi ya Mbagala, Temeke na Mkuranga.

“Kwa namna ya pekee tunaishukuru sana TANESCO kwa mradi huu, kwa awamu ya kwanza Mradi huu ulipaswa kujaribiwa mwezi Juni mwaka huu lakini Mradi umeweza kuonesha mafanikio kabla ya wakati kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa’’ alifafanua Mapunda.

Uboreshaji wa Mradi huu wa Kituo cha Kupokea na Kupoza na Kusambaza umeme cha Mbagala umegharimu Dola za Kimarekani milioni 6.4 ambapo sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake na kukamilika kwake kunatarajia kusambaza umeme wa Megawati 165.

spot_img

Latest articles

Mkataba wasainiwa kuwezesha gesi kuzalisha mbolea

Na Tatu Mohamed, Media Brain KATIKA juhudi za kukuza uzalishaji wa ndani wa mbolea na...

Mafanikio 10 ya Wizara na Utalii

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Maliasili na Utalii  imebainisha vipaumbele 10 ambavyo wizara na...

Wenye vyeti feki vya uandishi wa habari waonywa

Na Mwandishi Wetu, JAB WAKATI Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ikiufungua rasmi...

Waziri wa Mazingira wa Norway ateta na Waziri Masauni

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mha. Hamad Masauni...

More like this

Mkataba wasainiwa kuwezesha gesi kuzalisha mbolea

Na Tatu Mohamed, Media Brain KATIKA juhudi za kukuza uzalishaji wa ndani wa mbolea na...

Mafanikio 10 ya Wizara na Utalii

Na Mwandishi Wetu WIZARA ya Maliasili na Utalii  imebainisha vipaumbele 10 ambavyo wizara na...

Wenye vyeti feki vya uandishi wa habari waonywa

Na Mwandishi Wetu, JAB WAKATI Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) ikiufungua rasmi...